Kampuni za simu zinazotoa huduma ya fedha kwa njia ya simu za mkononi katika kipindi cha miezi miwili iliyopita Novemba na Desemba mwaka jana zimekusanya kiasi cha Sh. trilioni 13.07.
Kaimu Meneja wa Habari  Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Semu Mwakyanjala amesema kuna ongezeko kubwa la matumizi ya huduma za kifedha kwa njia ya mtandao hapa nchini.
Amesema kuwa katika miezi miwili iliyopita mwaka jana ambapo Novemba walikusanya Sh.trilioni 6.47 na Desemba Sh.trilioni 6.60 jumla ya makusanyo yote ni sh. Trilioni 13.07  kuptia kampuni za simu zinazohusika na huduma ya miamala.
Alitaja kampuni  zilizohusika na maiamala hiyo ni pamoja na Zantel(Easy Pesa),Tigo (Tigo pesa), Vodacom(Mpesa), Aiterl(Airtel Money na Halotel (Halopesa).
Aidha aliwataka wananchi kujihadhari na utapeli unaofanywa kwa kutumia simu za mkononi huku mamlaka na vyombo vya usalama vinashughulikia suala hilo.