23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

KAMPUNI ZA SIMU ZAKUSANYA TILIONI 13 KUPITIA HUDUMA ZA FEDHA

TCRAKampuni za simu zinazotoa huduma ya fedha kwa njia ya simu za mkononi katika kipindi cha miezi miwili  iliyopita Novemba na Desemba mwaka jana zimekusanya kiasi cha Sh. trilioni 13.07.

Kaimu Meneja wa Habari  Mamlaka  ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Semu Mwakyanjala amesema kuna ongezeko kubwa  la matumizi  ya huduma za kifedha kwa njia ya mtandao hapa nchini.

Amesema kuwa katika miezi miwili  iliyopita mwaka jana  ambapo Novemba walikusanya Sh.trilioni 6.47 na Desemba Sh.trilioni 6.60 jumla ya makusanyo yote ni sh. Trilioni 13.07  kuptia kampuni za simu zinazohusika na huduma ya miamala.

Alitaja kampuni  zilizohusika na maiamala hiyo ni pamoja na Zantel(Easy Pesa),Tigo (Tigo pesa), Vodacom(Mpesa), Aiterl(Airtel Money na Halotel (Halopesa).

Aidha  aliwataka wananchi kujihadhari  na utapeli unaofanywa  kwa kutumia simu za mkononi  huku mamlaka na vyombo vya usalama vinashughulikia suala hilo.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles