32.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Kampuni ya Tigo yaingia makubaliano na Wakandi Group kunyanyua taasisi za fedha

Na Beatrice Kaiza, Mtanzania Digital

KAMPUNI za Tigo Tanzania na ile ya Wakandi Group AS ya Norway zimeingia makubaliano kwa lengo ili kurahisisha huduma za kifedha kidigitali kwa kupitia Tigo Pesa kwa SACCOS na Taasisi ndogondogo za kifedha zilizosajiliwa

kwa mujibu wa makubaliano hayo, Tigo Pesa itaunganisha jukwaa lake la malipo na Wakandi’s Credit Association Management System (CAMS) kwa ajili ya Saccos na Taasisi ndogo za fedha ili kudhibiti huduma zao kwa ufanisi wa kidigitali kwa urahisi na usalama zaidi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Novemba 12, 2021 katika tukio hilo Afisa Mkuu wa huduma za kifedha wa Tigo Pesa, Angelica Pesha alisema jukwaa hilo litawezesha kusaidia kuweka miamala ya Saccos katika jukwaa moja la kidigital.

“Saccos sasa zimekomaa zaidi na zinahitaji jukwaa la kisasa la usimamizi wa fedha hii ni kutokana na sababu kuwa wanahifadhi kiasi kikubwa cha fedha, wanatoa mikopo na kusimamia riba zake na ndio maana sisi kama Tigo Pesa tukachukua fursa hiyo kwa kushirikiana na Wakandi kuweka miamala yote ya Saccos katika mfumo wa kidigitali kote nchini.

“Wakandi ina idadi kubwa ya wateja katika eneo lote la Afrika Mashariki hivyo ushirikiano huu unatupatia faida ya kiushindani kuwafikia wote waliotengwa katika huduma hizi za fedha za Kidigitali hasa katika Saccos, kupitia mfumo huu wanachama wataweza kutumia akaunti zao za Tigo pesa kuchangia amana zao za Saccos na kurejesha mikopo kupitia katika mfumo huohuo,” amesema Pesha.

Upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Wakandi, Espen Kvelland amesema kwa sasa Saccos zimekomaa hivyo zinahitaji jukwaa la kisasa.

“Sisi, Wakandi, tunalenga kufikia viwango vipya zaidi kwa kutumia Tigo Pesa na kusaidia SACCOS kuingia katika mfumo wa kidigitali wa kifedha. Ni fursa kwetu kujiimarisha zaidi katika soko la Tanzania. Ushirikiano huu ni hatua muhimu katika safari yetu ya kutoa uzoefu usio na pesa barani Afrika,” amesema Kvelland.

Ili kupata huduma hiyo, Saccos na Taasisi ndogo za kifedha zinahitaji kusajiliwa na Wakandi Credit Association Management System (CAMS) kwa ajili ya wanachama wao, ambao ni wateja wa Tigo Pesa ili kukamilisha miamala yao bila matatizo kupitia menyu ya Tigo Pesa au kupitia Tigo Pesa App.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles