25.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

KAMPUNI YA MAFUTA YA PUMA YAWAKUMBUSHA MADEREVA KUZINGATIA SHERIA YA ZA USALAMA BARABARANI

*Puma yaungana na Umoja wa Mataifa kuadhimisha wiki ya nenda kwa usalama barabara

Na Mwandishi Wetu-Dar es Salaam

KAMPUNI ya Mafuta Energy Tanzania imeungana na Shirika la Umoja wa Mataifa kuadhimisha wiki ya usalama barabarani huku kampuni hiyo ikitoa wito kwa madereva nchini kuzingatia sheria za usalama barabarani kwa lengo la kuokoa maisha ya watoto.

Kwa mujibu wa Kampuni ya Puma ni kwamba moja ya vipaumbele vyao ni suala la usalama barabarani ndio maana imeona umuhimu wa kuungana na shirika hilo kubwa duniani kuadhimisha siku hiyo kwa kutoa elimu kwa madereva wa vyombo vya moto nchini Tanzania.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania, Dominic Dhanah amewaambia waandishi wa habari kuwa wameamua kuitumia siku hiyo kutoa elimu kwa madereva ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Kimataifa ya Nenda kwa Usalama Barabarani ‘UN-Global Road Safety Week (UNGRSW).’

“Puma tumeungana na shirika hili kutoa elimu, ambapo kwetu Tanzania imetoa wanafunzi wa Shule ya Msingi na Bunge ambao ni mabalozi wa elimu ya usalama barabarani hususani kwa mkoa wa Dar es Salaam.

“Pia tumeamua kuwatumia watoto kutoa elimu ya usalama barabarani lengo letu Puma ni  kuhakikisha wanaanza kupata uelewa kuhusu masuala ya usalama barabarani,” amesema Dhanah.

Kwa upande wake Meneja Programu wa usalama barabarani,  Neema Swai amesema kauli mbiu ya mwaka huu ni ‘Sema Usikike, Okoa Maisha’ na kufafanua maadhimisho hayo huadhimishwa kila baada ya miaka miwili.

“Kila siku watoto ndio wanaotumia barabara kwenda shule na kurudi nyumbani, wasipokuwa na elimu ya kutosha tutawapoteza wengi.

Mmoja wa wanafunzi walioshiriki kutoa elimu, Godbless Mlacha anayesoma darasa la sita katika Shule ya Msingi Bunge, amesema wanawashauri  madereva kuacha kutumia vilevi au kwenda mwendo kasi wakiwa barabarani kwa kuwa maisha yao yanakua hatarini.

“Nahitaji kuishi ili nitimize ndoto zangu, uzembe wa dereva unaweza kuondoa uhai wangu au kunipa kilema cha kidumu. Nimechagua kupaza sauti ili kumaliza hili tatizo,” amesema Mlacha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles