24.5 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

Kakobe aibukia kanisani kwa Gwajima, amtetea sakata picha za faragha

LULU RINGO, DAR ES SALAAM

Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship, Zachary Kakobe, ameibuka katika Kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Askofu Josephat Gwajima na kukanusha kuwa video za faragha zinazosambaa mitandaoni zikimuonyesha Askofu huyo kuwa si za kweli.

Akizungumza katika ibada iliyofanyika katika kanisa hilo leo Jumapili Mei 12, Kakobe amesema vitabu vya dini haviamini ushahidi wa picha isipokuwa mashahidi watakaozungumza juu ya ukweli wa tukio husika.

“Yuko wapi huyo mshitaki mpaka sasa, mbona hayupo amefutika na kama hayupo huo tunauita unafiki, mshitaki wa Gwajima yuko wapi ? Polisi ndio wanamtafuta sasa hivi, sasa kama una ushahidi wa halali kwanini unajificha.

“Hatukubali Mashitaka juu ya Askofu Gwajima isipokuwa kwa vinywa vya mashahidi wawili watatu watakaosimama na kuthibitisha juu ya video ile,” amesema Askofu Kakobe.

Aidha Askofu Kakobe amesisitiza mshikamano kati ya viongozi wa makanisa ya kiroho pamoja na viongozi wa serikali akiwamo Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Paul Makonda na kusema anaamini Kiongozi huyo anapenda umoja hivyo hawezi kupenda matengano kati yao.

“Askofu Gwajima ana roho wa Mungu ndani yake, Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda ana roho wa Mungu ndani yake hawawezi kupenda matengano isipokuwa watu wasio na roho wa Mungu kama hawa walioleta hii video,” amesema Askofu Kakobe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles