24.5 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Kampuni ya KCL, Agri-Ajira zajitosa kwenye kilimo

Mwandishi Wetu

Kampuni ya Agri-Ajira imewapa changamoto ya kujitosa kwenye kilimo cha biashara Kampuni ya KCL Ltd. kutokana na mafanikio waliyopata ikiwamo kujiajiri.

Kampuni hiyo inayoundwa na vijana wawili, Ibrahim Charles na Samwel Jonathan, imekuwa chachu kwa Kampuni ya KCL Ltd na vijana wengine nchini kutokana na kuthubutu kwao na kuwa mfano kwa vijana baada ya kujitosa kwenye kilimo na kulima kwa mafanikio makubwa ekari 50 za mpunga katika Kata ya Rutinda, Wilaya ya Kilosa, mkoani Morogoro.

Vijana hao kutoka katika kampuni hizo mbili wamekutana leo katika Siku ya Mavuno mkoani Morogoro ambapo mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu, Anthony Mavunde.

Licha ya mafanikio hayo vijana hao wamesema, changamoto zilizopo ni upatikanaji wa maeneo ya kilimo, uwezeshaji kwa vijana mathalani katika pembejeo na mikopo ya mitaji ya uwekezaji ambapo wametoa maombi kwa serikali kuwashika mkono vijana ili waweze kuwa chachu si tu ya kujiajiri ila kuzalisha fursa za ajira kwa vijana wengine.

Kwa upande wake Mavunde aliahidi kushughulikia changamoto hizo kwa kushirikiana na Benki ya Maendeleo ya Kilimo nchini (TADB) kuwawezesha vijana na kuagiza uongozi wa mkoa na Wilaya ya Kilosa kuhakikisha unatafuta na kutenga maeneo kwa vijana hao.

“Niwasihi na vijana wengine wajiunge na kilimo na kuhakikisha kilimo kinaleta tija nchini ili kupunguza umasikini, upatikanaji wa ajira na kuongeza upatikanaji wa chakula nchini,” amesema Mavunde.

Naye mmoja ya Wakurugenzi wa KCL, Gabriel Munasa, amesema amejifunza mengi ambapo ameahidi kutumia maarifa aliyopata kwa niaba ya KCL kuhamisha maarifa hayo kwa kampuni yao ya vijana waliotokana na Group ya WhatsApp na kuwa kampuni katika kufikia malengo mengi waliyo nayo kama kampuni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles