26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, January 8, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

KAMPUNI YA BOEING YASHTAKIWA KWA AJALI YA SHIRIKA LA NDEGE LA ETHIOPIA

Kampuni ya utengenezaji ndege ya Boeing imefunguliwa mashtaka nchini Marekani na familia ya moja ya abiria waliofariki kwenye ajali ya Shirika la Ndege la Ethiopia.

Watu wote 157 waliokuwa ndani ya ndege hiyo walifariki katika ajali hiyo iliyotokea mapaema mwezi huu.

Ndugu wa Jackson Musoni, ambaye alikuwa ni mfanyakazi wa Umoja wa Mataifa na raia pekee wa Rwanda aliyekuwemo kwenye ajali hiyo, wanadai kuwa ndege sampuli ya Boeing 737 Max zinamapungufu ya kiusanifu katika mifumo yake ya kujiendesha.

Ndege zote 371 zinazomiikiwa na mashirika mbalimbali za aina ya 737 Max zimepigwa marufuku kuruka toka ilipotokea ajali hiyo, ambayo ilikuwa ni ya pili kwa sampuli hiyo ndani ya miezi mitano. Ajali ya kwanza ilitokea mwezi Oktoba 2018 nchini Ethiopia na kuua watu wote 181 waliokuwamo ndani.

Kampuni ya Boeing bado haijatoa tamko lolote kuhusu kesi hiyo.

Wachunguzi pia bado hawajatoa ripoti kamili juu ya sababu hasa ya ajali hiyo kutokea.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles