21.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, July 23, 2024

Contact us: [email protected]

Kampuni ya Ally’s Star yapewa onyo Simiyu

Na Mwandishi wetu, Simiyu

Kampuni ya mabasi ya Ally’s Star ya mkoani Shinyanga imepewa onyo la mwisho na uongozi wa Mkoa wa Simiyu, kwa kile kilichodaiwa kutoa huduma mbaya kwa wateja wake ikiwemo lugha zisizokuwa na staha kwa abiria.

Kampuni hiyo ambayo baadhi ya magari yake ya kubeba abiria (basi) ufanya safari zake kutoka Mkoani Simiyu (Bariadi) hadi Dar es Salaam, ambapo abiria kutoka mkoani Simiyu wamekuwa wakilalamikia juu ya huduma mbovu za magari hayo.

Moja ya kero kubwa inayodaiwa kulalamikiwa abiria wengi ni suala la kufaulishwa bila ya utaratibu, huku ikiambatana na lugha mbaya endapo abiria wanapoonza kulalamikia utaratibu huo.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dk. Yahya Nawanda jana kwenye maazimisho ya wiki ya nenda kwa usalama Barabarani yaliyofanyika mjini Bariadi, alitoa onyo la mwisho kwa kampuni.

Dk. Nawanda alisema kuwa ikiwa Kampuni hiyo wataendeleza utaratibu huo watapigwa marufuku kufanya kazi mkoani humo, kwa kile alichoeleza kuwa malalamiko kwake yamekuwa mengi.

Alisema kuwa baadhi ya magari ya kampuni hiyo ufanya safari zake kutoka Bariadi kwenda Dodoma na Morogoro, ambapo wakati wa kutoka kwenye mikoa hiyo kuja Bariadi abiria hao ukalishwa Mkoani Shinyanga wakisubilia basi la kampuni hiyo kutoka Dar es Salaam.

“Watu wanatoka Morogoro na Dodoma kuja Bariadi, wakifika Shinyanga saa 10:00 jioni, wanakalishwa Shinyanga mpaka saa nne usiku wakisubilia basi la kampuni hiyo kutoka Dar es Salaam,” alisema Dk. Nawanda.

“Wanawakalisha Shinyanga muda mrefu…kwanza wanawapotezea muda, lakini abiria hawapewi chakula wala chai kama ilivyosheria, abiria wakianza kulalamika wanatolewa lugha mbaya,” aliongeza Dk. Nawanda.

Mkuu huyo wa Mkoa aliagiza Mamlaka ya udhibiti usafiri ardhini (LATRA) Mkoani humo kufanya uchunguzi dhidi ya tuhuma hizo na kumchukulia hatua kali mmiliki wa magari hayo.

“Waambieni wahusika, waache mara moja hii tabia, malalamiko sasa yamekuwa mengi, ikiwa wataendelea nitachukua hatua kali ya kuwazuia kufanya biashara kwenye mkoa huu, hatuwezi kuwa na watu wanaonyanyasa wananchi,” alisema Dk. Nawanda.

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Simon Simalenga naye alisema kuwa amepata malalamiko ya magari ya kampuni hiyo ambapo alimtaka mmilikiwa wa magari hayo kujirekebisha mara moja.

“Kila mmoja amemsikia mkuu wa Mkoa akisema atawazuia kufanya kazi ndani ya mkoa ikiwa wataendelea, sasa mimi nasema kabla ya Mkuu wa Mkoa kufanya hivyo, mimi nitawapiga marufuku kufanya kazi ndani ya Wilaya ya Bariadi.

“Nimsihi mmiliki wa haya magari, kama anaipenda kazi yake basi aache mara moja huu utaratibu, mimi huwa sishindwi jambo, nikiamua nafanya kweli, narudia tena waache mara moja,” aliongeza Simalenga.

Ofisa Mfawidhi kutoka LATRA mkoani humo, Niclous Kamzora alikiri ofisi yake kupata malalamiko kutoka kwa abiria dhidi ya magari ya magari ya kampuni hiyo na walianza kuyafanyia kazi.

“Tulipata hayo malalamiko, tukamwandikia barua ya onyo na tukimtaka atoe maelezo, sasa leo Mkuu wa Mkoa ametoa maelekezo kwetu, na inavyoonekana kampuni hii imerudia makosa, tunakwenda kufuatilia na ikibainika tutachukua hatua kali,” alisema Kamzora.

Hata hivyo, tulimtafuta msimamizi wa magari hayo Abdallah Abdallah ambaye alisema kuwa tuhuma hizo dhidi ya kampuni yao hazina ukweli, bali ni vita ya kibiashara kutokana na ukubwa wa kampuni yao.

Abdallah alisema kuwa siyo kweli kuwa abiria ufaulishwa kila mara, bali utokea mara moja ikiwa gari moja likipata itirafu ya kiufundi, basi abiria utakiwa kusubilia gari nyingine ili waweze kufikishwa salama.

“Hili jambo ni mara moja tu, hatuwezi kusafirisha abiria na gari mbovu, tukiona hili gari limekuwa na itilafu, basi tunawaomba abiria kusubilia gari lililoko nyuma ili kuwafikisha salama.

“Suala la lugha mbaya nalo siyo kweli, ndiyo maana magari yetu mpaka sasa yanapata abiria wengi kutoka Bariadi, waswahili walitufundisha wakasema hivi…ukoo mkubwa na misiba mingi…asante,” alisema Abdallah.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles