24.8 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Kampuni ya AAR yapongezwa kwa huduma bora

Na MWANDISHI WETU

-DODOMA

KAMISHNA wa Mamlaka ya Bima Tanzania (TIRA), Dk. Baghayo Saqware, ameipongeza Kampuni ya Bima ya AAR kwa jinsi inavyojitolea kusaidia jamii na kutoa huduma bora. 

Pongezi hizo alizitoa juzi jijini Dodoma katika hafla ya futari iliyoandaliwa na AAR ambayo ilihudhuriwa na wabunge, viongozi wa dini, bodi ya wakurugenzi wa AAR na wawakilishi wa watoa huduma za Bima. 

“Kwa dhati, niwapongeze AAR kwani wamekuwa mstari wa mbele kujitolea kufanya shughuli za kijamii kama kusaidia watoto yatima, wazee, walemavu na hata kusaidia kuhuisha ubora wa mazingira yetu. 

“Na sasa juhudi zao zimefanikisha uwepo wetu katika kushiriki iftari itakayohamasisha ari na moyo wa kujitoa zaidi kwa jamii,” alisema Dk. Saqware. 

Pamoja na hali hiyo, alitoa wito kwa makampuni mengine pamoja na watu binafsi kuiga mfano wa AAR na kujitolea kuhuisha ubora wa maisha ya jamii kadiri wawezavyo, ikiwa ni kuakisi kipindi cha mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. 

Alizitaka taasisi zote zinazotoa huduma za Bima kuzingatia matakwa ya sheria na kujikita katika kutoa huduma bora na kushiriki katika kuzuia udanganyifu katika sekta ya bima. 

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa AAR, Violet Modichai, aliwashukuru wabunge kwa kuhudhuria tukio hilo na kueleza kuwa wameamua kutumia Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kuwakutanisha  viongozi hao ambao ni wawakilishi wa wananchi pamoja na wadau wa bima ili kukumbushana kuhusu umuhimu wa kujitolea kwa jamii pamoja na kutii sheria na maelekezo ya vitabu vitakatifu. 

“Tunaahidi kuendelea kutoa msaada zaidi kadiri tuwezavyo. Pia, tunahakikisha tunaendelea kutoa huduma bora zaidi zinazojenga Taifa lenye afya na lenye uhakika wa kulinda maendeleo ya kila mmoja kupitia bima,” alisema Modichai. 

Akizungumza baada ya futari hiyo, Mbunge wa Maswa Magharibi ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti ya Bunge, Mashimba Ndaki (CCM), aliishukuru AAR kwa kuandaa tukio hilo. 

“Mheshimiwa mgeni rasmi, sisi kama wabunge na familia zetu tunafaidika na huduma za bima ya afya. Kwa hiyo, niwapongeze watoa huduma kwa kuturahisishia maisha yetu. Badala ya kuhangaika kutafuta fedha wakati nimeugua, wao wananisaidia kwa kuwa nimeshalipa kabla,” alisema. 

Mbunge huyo alisema anaridhishwa na huduma ya bima za afya, alitoa ombi lake kwa makampuni ya bima kuangalia uwezekano wa kupunguza zaidi gharama za bima za afya ili wananchi wengi zaidi waweze kujiunga.  

Aliwaomba AAR kupeleka huduma ya bima ya afya vijijini ili kuwasaidia pia wananchi walioko katika maeneo hayo kufaidika na ubora wa huduma hizo. 

“Mwaka huu, AAR iliyokuwa inatoa huduma ya afya pekee, ilianzisha utoaji wa huduma za jumla kutokana na maombi ya wananchi waliohitaji huduma zao kwenye maeneo mengine.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles