26.9 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 5, 2023

Contact us: [email protected]

Mipango ya kusafirisha mwili wa Etienne Tshisekedi yaahirishwa

Mipango ya kuusafirisha mwili wa aliyekuwa kiongozi wa upinzani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Etienne Tshisekedi, kutoka Ubelgiji hadi mjini Kinshasa, iliahirishwa  dakika ya mwisho jana jioni.

Ofisa mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwe, aliliambia shirika la habari la AFP kwamba kuahirishwa huko kulitokana na matatizo katika mpangilio wa safari.

Ubelgiji ilikuwa imeandaa gwaride la kijeshi kumuaga marehemu Tshisekedi, baba wa rais wa sasa Felix Tshisekedi, na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ubelgiji Didier Reynders alikuwa tayari uwanjani.

Taarifa kutoka familia ya Tshisekedi zimeeleza kuwa safari ya kumrejesha marehemu mjini Kinshasa imehamishiwa saa nane mchana wa leo, kutoka uwanja binafsi wa ndege karibu na Brussels.

Etienne Tshisekedi alifariki Februari 1, 2017, lakini mwili wake ulisalia huko kutokana na tofauti kati ya familia yake na serikali ya wakati huo, kuhusu hadhi ya mazishi yake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles