26.5 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

KAMPUNI BINAFSI ZA ULINZI KUVAA SARE MOJA

Na Bethsheba Wambura, Dar es Salaam

Kampuni binafsi za ulinzi zinazoendesha shughuli zake nchini zimetakiwa kuvaa sare za aina moja ifikapo Januari Mosi mwakani ili kuondoa sare zinazofanana na za askari wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama.

Agizo hilo limetolewa leo Jumanne Machi 13, jijini Dar es Salaam na Kamishna wa Kamisheni ya Ushirikishwaji wa Jamii, Mussa Mussa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika kikao kilichowakutanisha wamiliki wa kampuni binafsi za ulinzi.

Kamishna Mussa amesema sare zilizokubaliwa kwa pamoja kati ya Jeshi la Polisi na wawakilishi wa kampuni binafsi za ulinzi zinatakiwa ziwe na rangi ya bluu nyeusi (Dark blue), nyeusi pamoja na mashati meupe kulingana na mazingira ya kampuni inapofanyia ulinzi.

“Kampuni zote binafsi za ulinzi hakikisheni mnajiandaa mapema kwa kuwa muda utakapofika hakuna kampuni binafsi ya ulinzi itakayoruhusiwa kufanya kazi bila ya kutumia sare hizi ambazo zitakuwa ni utambulisho rasmi wa sekta hii binafsi ya ulinzi,” amesema Mussa.

Kwa upande wake Katibu wa Chama cha Wamiliki wa Kampuni Binafsi za Ulinzi (TAPSCOA), Shawiniaufoo Kimuto amesema kuwepo kwa aina moja ya sare kutasaidia kuondoa mgongano uliopo hivi sasa ambapo baadhi ya kampuni zinavaa sare zinazofanana na zinazovaliwa na vyombo vya ulinzi na usalama.

“Hatua hii itasaidia kufahamika kwa urahisi kwa walinzi wa kampuni binafsi na hivyo kuwa rahisi kupata msaada pindi wanapotekeleza majukumu yao ya kulisaidia Jeshi la Polisi kuhakikisha usalama unakuwepo katika maeneo wanayofanyia kazi,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles