28.2 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Kampuni 16 zakubali kufilisiwa

kevelaNA SHABANI MATUTU, DAR ES SALAAM

MALI za kampuni 16 zilizokwepa kodi zinatarajiwa kutaifishwa   ndani ya wiki moja baada ya kushindwa kulipa kodi ya makontena yao bandarini.

Kampuni hizo zilishindwa kulipa fedha hizo  ndani ya siku 14 zilizokuwa zimetolewa  na Kampuni ya udalali ya Yono Auction Mart kwa kushirikiana na Mamlaka ya  Mapato Tanzania (TRA).

Kati ya kampuni hizo nane, mbili ambazo ni Tifo Global Trading Co.ltd na Lotai Steel Tanzania ltd zilikubali kushirikiana na Yono kutaifishwa mali zao  kuhakikisha deni la kodi waliyokuwa wamekwepa linalipwa.

Kwa mujibu wa notisi iliyotolewa na Kampuni hiyo ya udalali, kampuni 24 zilizobainika kukwepa kodi TRA, zilitakiwa ziwe zimelipa deni hilo hadi kufikia juzi, lakini kati ya hizo ni nane pekee ambazo zimefanya hivyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni hiyo, Yono Kevela, alisema   kodi inayodaiwa kwa kampuni zote 24 ni Sh  bilioni 18.9.

Yono alisema hadi sasa kampuni yake imekamata mali zenye thamani ya Sh  bilioni sita, huku ikitarajia hadi jana jioni ingekuwa imekamata mali nyingine zenye thamani ya  zaidi ya Sh  bilioni saba.

“Tangu tumetoa siku 14, hadi sasa zimekwisha kulipwa zaidi ya Sh  milioni 200 za kodi hiyo na tunatarajia ndani ya wiki moja ijayo serikali itakuwa imepata kodi yake yote ambayo ilikuwa inazidai kampuni hizo.

“Hata hizo kampuni zilizobaki lazima zitalipa na zile tutakazozikosa tutawakamata wamiliki wa bandari kavu ya Azam ICD na kampuni ya usafirishaji, upakiaji na upakuaji mizigo ya Reginal Cargo Ltd ambako makontena 329 yalipitia mikononi mwao,” alisema na kuongeza

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles