25.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

KAMPENI YA KATA UMEME YAIPA TANESCO BIL 41/-

Na ASHABANI

-DAR E SALAAM

SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco) limekusanya madeni sugu ya  Sh bilioni 41 kutoka taasisi za serikali na binafsi.

Akizungumza na waandishi wa habari  Dar es Salaam jana, Meneja Mwandamizi Hesabu wa Tanesco, Philidon Siyame alisema hatua hiyo imetokana na mafanikio yaliyopatikana chini ya Rais Dk. John Magufuli kutokana na utendaji wake.

Alisema wakati Rais Magufuli anaingia madarakani kulikuwa na deni la Sh  bilioni  275 ikiwa deni la Shirika la Umeme Zanzibar ( ZECO), lilikuwa linadaiwa bilioni 180 taasisi binafsi bilioni 95  ambazo kwa kiasi kikubwa wamefanikiwa kuzilipa.

“Machi mwaka huu deni lilikuwa Sh bilioni 275 ambako ZECO walikuwa wanadaiwa ni Sh bilioni 180 na taasisi binafsi Sh bilioni 95 baada ya kampeni ya kata iliyotangazwa na Rais Magufuli akiwa Mtwara tumekusanya Sh bilioni 41 ambayo ZECO wamelipa ni Sh bilioni 18 kati Sh bilioni 180 walizokuwa wakidaiwa na taasisi nyingine za serikali Sh bilioni 18 huku taasisi binafsi Sh bilioni tano makusanyo yamekuwa na mafanikio makubwa,’’alisema Siyame.

Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa shirika hilo, TUICO, Hassan Athumani alisema hawana budi kumpongeza Rais Dk. Magufuli kwa utendaji wake kwa kufanikiwa kutoa maagizo yaliyotekelezwa kwa weledi.

“Kampeni ya ‘KA-TA’ iliyoasisiwa na Rais  imeweza kukusanya deni la umeme kwa kiasi kikubwa jambo ambalo hapo awali haikuwa rahisi kwa maana kuwa kabla ya agizo lake tulikuwa na uwezo wa kukusanya mapato ya shirika kwa asilimia 90 kwa mwezi lakini kwa sasa ni asilimia 104 ya deni lote la wadaiwa sugu,’’alisema Athumani.

Alisema  wameshuhudia mafanikio katika uanzishwaji na uendelezwaji wa miradi ya mikakati kama vile mradi mkubwa wa kufua umeme wa gesi asilia wa Kinyerezi II utakaozalisha Megawati 240.

Alisema awamu ya kwanza ya mradi huo utakamilika Desemba mwaka huu na  umeme huo utaingizwa kwenye gridi ya taifa sambamba na upanuzi wa mradi wa Kinyerezi I wenye ambao una uwezo wa kuzalisha Megawati 185 za umeme.

Licha ya hali hiyo alisema  a mradi wa usafirishaji wa umeme  North East Grid utakaoanzia Dar es Salaam, Chalinze hadi Arusha wa msongo wa Kilovolti 400 pamoja na mradi wa usafirishaji umeme Kilovolti 220 kutoka Makambako hadi Songea.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles