29.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 20, 2024

Contact us: [email protected]

Kampeni dhidi ya ugonjwa wa usonji yazinduliwa

????????Na Veronica Rwamwald, Dar es Salaam

KLINIKI ya Lotus kwa kushirikiana na Hospitali ya Taifa Muhimbili, imeanzisha kampeni mpya inayolenga kuelimisha umma kuhusu ugonjwa wa usonji (autism), ambao Watanzania wengi hawaufahamu.

 

Ugonjwa huu sasa unatishia familia nyingi kwani dalili zake huanza utotoni na zinaweza kuendelea hadi ukubwani.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Chama cha Kuhudumia watu wenye usonji Tanzania, Dk. Stella Rwezaula,

aliishukuru Kliniki ya Lotus kwa kuwa mstari wa mbele kuanzisha kampeni  hiyo ili kuwaelimisha Watanzania kuhusu ugonjwa huo.

“Ni vyema ugonjwa huu ukigundulika mapema na kutibiwa ili aliyeathirika aweze kupona na kuishi maisha ya kawaida hapo baadaye kulingana na athari aliyoipata. Mtoto kuanzia miaka 0-6 anaweza kutibiwa vizuri na kusaidia kubadilisha maisha yake,” alisema.

 

Alisema watoto wenye hali hiyo wana shida katika kuwasiliana na tabia zao ni kurudia rudia mambo anayofanya mara kwa mara na pia watu wengi wenye ugonjwa huu wana namna yao ya kujifunza, kusikiliza na kuitika.

“Mfano wa hali hii ni kwamba, katika hali ya kawaida mtoto wa mwaka mmoja hutabasamu au kuwa na furaha kila  wakati, huiga mambo mbalimbali anayoona na kufuatilia vitu anavyoviona vikisogea, lakini mtoto mwenye ugonjwa huu hafanyi vitu hivi,” alisema.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kliniki ya Lotus, Dialla Kassam, alisema uelewa bado ni mdogo nchini Tanzania na watoto wengi huathiriwa na

kuja kujulikana wakati hali imeshakuwa mbaya zaidi.

“Kukosa uelewa wa hali hii ya watoto wenye mahitaji huwafanya walimu

na wazazi kudhani watoto ni watundu, wavivu au wanakera na wakati mwingine huadhibiwa kwa sababu hiyo wakati watoto hawa wanahitaji uangalizi wa karibu, kupendwa na kupata msaada kutoka kwa walimu na wenzao,” alisema.

Alisema kliniki mbalimbali kuhusu ugonjwa huo hufanyika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kila Alhamisi na kwamba Chama cha Watu

Wenye Usonji-Tanzania (NAPA-T) kimekuwa kikisaidia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles