25.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Kamisha TRA aeleza sababu makusanyo kupanda maradufu

 MWANDISHI WETU -MBEYA 

KAMISHNA Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Dk. Edwin Mhede, amesema kwa sasa makusanyo kwa mwezi ni Sh. trilioni 1.5 ambazo ni ongezeko la asilimia 76 ikilinganisha Sh bilioni 850 zilizokuwa zikikusanywa kwa mwezi kabla ya Serikali ya awamu ya tano. 

Alisema hayo juzi jijini Mbeya wakati wa kikao kazi cha tathmini ya utendaji kazi wa Idara ya Kodi za Ndani. 

Alisema jitihada za Serikali ya awamu ya tano katika ngazi zote imechangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la makusanyo hayo ikiwa ni pamoja na kuzuia mianya ya ukwepaji kodi, kuhamasisha matumizi ya mashine za kielektroniki (EFD) na kudhibiti nidhamu na uadilifu kwa watumishi wa TRA. 

“Pia miradi mikubwa ambayo inatekelezwa na Serikali katika maeneo mbalimbali nchini kwa kutumia mapato ya ndani imekuwa ni chachu ya kuhamasisha ulipaji kodi kwa hiari kwa kuwa walipakodi wanaona thamani ya kodi wanayolipa,” alisema Dk. Mhede. 

Alisema TRA imekuwa ikichukua hatua mbalimbali katika kuhakikisha watumishi wake wanafanya kazi kwa uadilifu na uwajibikaji na kwamba katika kuhakikisha suala la maadili linazingatiwa, mamlaka hiyo imeunda idara maalum inayosimamia maadili na uadilifu wa watumishi hao. 

Alisema lengo la kikao hicho ni kutathmini utendaji kazi wa idara hiyo kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2019/20 na kujadili mikakati mipya ya mwaka wa fedha 2020/21 ili kuongeza ufanisi katika ukusanyaji mapato.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles