24.4 C
Dar es Salaam
Thursday, October 31, 2024

Contact us: [email protected]

Kambi ya Skauti kujengwa Dodoma

Na Mwandishi Wetu, Mwanza

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imefanikiwa kupata eneo la ujenzi wa kambi ya Skauti yenye hadhi ya Kimataifa katika eneo la Chigongwe jijini Dodoma.

Hayo yameelezwa jijini Mwanza Jana na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omari Kipanga (Mb) alipomuwakilisha Rais wa Skauti ambaye pia ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda (Mb) katika maadhimisho ya Siku ya Mwanzilishi wa Skauti Duniani, Sir Baden Powel.

Amesema Wizara kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI imewezesha utoaji wa mafunzo kwa walimu walezi wa Skauti wapatao 300 wa shule za Msingi na Sekondari.

“Niwahakikishie kuwa Wizara itaendelea kutoa mafunzo haya kwa walimu ambao bado hawajayapata,” amesema Kipanga.

Aidha, Kipanga ametoa rai kwa viongozi wote wa Chama cha Skauti Tanzania ngazi ya Taifa, Mkoa na Wilaya kuthamini dhamana kubwa waliyopewa ya malezi ya vijana wa Kitanzania na kuwaasa kuyaishi maneno yaliyotamkwa na mdhamini wa chama hicho mwaka 2018, Alhaji Ali Hassan Mwinyi yenye ujumbe wa ‘maisha yetu ni hadithi.’

“Ningependa kila skauti ayaishi maneno haya ili kuepuka tabia za aibu zenye kudhalilisha utu wa mtu tukiwa tumebeba sura ya wengi tunaowawakilisha,” amesema Naibu Waziri Kipanga.

Naibu Waziri Kipanga amewapongeza Skauti hao kwa kuadhimisha siku hiyo kwa kuacha alama kwenye jamii na Taifa kwa ujumla na kawahimiza kuendelea kuziishi kanuni na kiapo cha Skauti kwani ndizo zinazowatofautisha wao Taasisi nyingine.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles