27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 13, 2024

Contact us: [email protected]

Kamati za Bunge kutangazwa wakati wowote

owenSHABANI MATUTU, DAR ES SALAAM

KAMATI za Bunge zinatarajiwa kutangazwa wakati wowote kuanzia sasa, kabla ya mkutano wa pili wa Bunge la 11 kuanza Januari 26, MTANZANIA limebaini.

Taarifa za uhakika kutoka ndani ya Ofisi za Bunge zimelieleza gazeti hili kwamba, suala hilo lipo jikoni na wiki hii Spika anatarajiwa kutangaza kamati za Bunge.

Akizungumzia hilo jana jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Habari, Owen Mwandumbya alikiri suala la kamati za Bunge kushughulikiwa na Spika, Job Ndugai, huku akisisitiza kuwa suala hilo lipo katika hatua nzuri.

“Spika anashughulikia suala la kamati naamini hivi karibuni zitakuwa zimekamilika na kutangazwa hadharani hata kabla ya kuanza kwa Bunge lijalo,” alisema Owen.

Kamati hizo zinatarajiwa kutangazwa mapema kwa sababu kabla ya kuanza kwa Bunge Januari 26 taratibu zinataka kamati za Bunge zianze kwanza mikutano yake.

Muundo wa kamati

Kamati za Bunge huundwa kwa mujibu wa Katiba Ibara ya 96, likiwa limepewa madaraka ya kuunda kamati za Bunge za aina mbalimbali na muundo wake umefafanuliwa na Kanuni za Kudumu za Bunge.

Katika muundo huo zipo kamati za kisekta na zile zisizokuwa za kisekta, ambazo kwa pamoja hufanyakazi na kutekeleza majukumu yao kwa niaba ya Bunge.

Kwa mujibu wa Kanuni ya 89 Bunge limeunda Kamati 15 ambazo ni Kamati ya Uongozi, Kamati ya Fedha na Uchumi, Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala, Kamati ya Uwekezaji na Biashara na Kamati ya Mambo ya Nchi za Nje.

Nyingine ni Kamati ya Kanuni za Bunge, Kamati ya Ulinzi na Usalama, Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, Kamati ya Huduma za Jamii na Kamati ya Maliasili na Mazingira.

Nyingine ni Kamati ya Maendeleo ya Jamii, Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), Kamati ya Kilimo na Ardhi pamoja, Kamati ya Miundombinu na Kamati ya Huduma za Jamii.

Hata hivyo kanuni ya 88 (12) imetoa fursa kwa kila kamati kuunda kamati nyingine ndogo kwa ajili ya uendeshaji bora wa shughuli zake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles