23.6 C
Dar es Salaam
Saturday, May 18, 2024

Contact us: [email protected]

Kamati yashauri bunge kufanya marekebisho ya sheria ya ndoa…

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria imesema umefika wakati muafaka wa Bunge kufanya marekebisho ya sheria ya ndoa ya mwaka 1971 hususan vifungu  vya  13 na 17  kwa kuwa vimepitwa  na wakati  kwani inatoa idhini ya watoto wa kike kuolewa wakiwa chini ya umri wa miaka 18.

Akizungumza Jumamosi  April 17, 2021 wakati wa majadilino yaliyoandaliwa na Taasisi ya Msichana Initiative  juu ya vifungu vya 13 na 17 vya sheria ya ndoa,Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo,Najma Giga amesema  sheria hiyo imekuwa na mapungufu makubwa hivyo watajitahidi iweze kufanyiwa marekebisho hususani kifungu cha 13 na 17.

“Sasa umefika muda muafaka sheria hii kuangaliwa na sisi Wabunge tunatakiwa kupaza sauti na kuifanyia marekebisho sheria hii kwani watoto wetu wa wanaolewa katika umri wa chini ya miaka 18 na mfano ni kwangu mwenyewe mama yangu aliolewa akiwa na umri wa miaka 14,”amesema.

Kwa upande wake, Mbunge wa Manyoni Magharibi, Elibariki Kingu (CCM) amesema kifungu hicho kimekuwa kichaka cha baadhi ya watu kuficha mambo yao kwani kuna baadhi ya mabinti wamekuwa wakipewa mimba na kisha wahusika kuwaoa ili kuficha makosa yao.

“Tunataka sheria isimame kwa wote kuwalinda watoto wa kike na wa kiume unakuta mtoto anapewa mimba akiwa chini ya umri wa miaka 18 na kisha mhusika anamuoa kwa kisingizio cha sheria hiyo,”amesema.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Msichana Initiative, Rebeca Gyumi amesema  mara baada ya wao kupaza sauti sasa ni zamu ya Wabunge kuhakikisha vifungu hivyo vinafanyiwa marekebisho ili umri wa mtoto wa kike kuolewa uwe kuanzia miaka 18.  

“Kamati hii ni muhimu kama wadau tumekuja kuongea nao ili tuweze kurekebisha kipengele cha 13 na 17 kinachoruhusu mtoto  wa kike kuolewa kuanzia miaka 18 na kuweka umri wa usawa kwa mtoto  wa umri wa miaka 18, tunaamini kutokana na mazungumzo yetu kamati imetusikiliza tunasema siku zote ni zamu ya wabunge kwahiyo tupo tayari kutoa sauti,”alisema.

Naye, Mbunge wa Viti Maalum,ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Katiba na Sheria Asha Abdalla Juma ‘Mshua’ (CCM)  alisema umefika muda muafaka wa kupiga vita mila potofu na kumsaidia mtoto wa kike kuingia katika ndoa akiwa anajitambua.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles