24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Kamati yaridhishwa ujenzi wa mradi

Na Mwandishi wetu, Mwanza

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imetembelea na kukagua ujenzi wa mradi wa SGR kipande cha Isaka Mwanza ambapo imeridhishwa na hatua iliyofikiwa ya asiliamia 54.

Wakizungumza baada ya kukagua mradi  huo unaogharimu zaidi ya shilingi trilion 3 baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo akiwemo, Miraji Mtaturu na Stelleh Simon  wamesema kukamilika kwa ujenzi wa madaraja na maeneo ya vivuko ni hatua katika  maendeleo ya mradi.

“Tunaendelea kusisitiza na kuielekesa serikali iendelee kufanya jitihada ili mradi huu ukamilike kwa wakati wananchi waweze kunufaika nao maana wote tunajua faida ambazo wananchi watazipata,”amesema Stella na kuongeza;

“Nawasihi wananchi waitunze miundombinu hii ya reli wasilime kandokando ya reli ili kuepuka  kuharibu  miundombinu kwa sababu wakiendelea na shughuli za kilimo karibu na reli baada ya muda michanga itajaa na reli itakuwa haina kazi tena au mvua zinaweza zikanyesha sana zikabeba mchanga reli na madaraja vikabomoka,”amesema.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Nchini Masanja Kadogosa amesema kuwa namna ujenzi wa  SGR lots namba 5 Isaka Mwanza unavyoendelea unatarajiwa kukamilika mapema.

Kwa mujibu wa Kadogosa kampuni ya china civil engineering constuction corporation ndiyo wanaojenga kipande cha tano cha Isaka Mwanza na kwamba utakamilika kabla ya uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika mwaka 2025.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles