28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Array

Kamati kuzuia uhalifu baharini yakutana Dodoma

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Kamati ya Usimamizi wa Mradi wa Kukabilina na Vitendo vya Kihalifu katika Bahari na Maziwa Makuu imekutana na kufanya kikao cha dharura kwa lengo la kujadili mkataba wa ununuzi wa boti ya doria litakalosaidia kukabiliana na vitendo hivyo nchini.

Kikao hicho kimesimamiwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye pia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Dk. John Jingu katika ukumbi wa ofisi hiyo Mei 30, 2022 jijini Dodoma kikihusisha Makatibu Wakuu kutoka wizara mbalimbali na wadau wa maendeleo.

Miongoni wa wajumbe waliohudhuria ni pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Uchukuzi), Gabriel Migire, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Abdallah Kirungu, Naibu Mwakilishi Mkaazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mipango ya Maendeleo, Sergio Valdini na Mwakilishi wa Balozi wa Japan Tanzania, Tabuchi Tomoyoshi.

Naibu Mwakilishi Mkaazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mipango ya Maendeleo Bw. Sergio Valdini akichangia hoja wakati wa majadiliano katika kikao hicho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles