
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KAMATI Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CC) inatarakuwa kukutana kesho jijini Dar es Salaa chini ya Mwenyekiti wake Rais mstaafu Jakaya Kikwete.
Taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na Msemaji wa CCM, Christopher ole Sendeka, ilieleza kuwa kikao hicho pamoja pamoja na mambo mengine kitajadili masuala kadhaa ya chama hicho ikiwa kutangazwa kwa tarehe ya mkutano mkuu maalumu.
Katika mkutano huu inatarajiwa Kikwete, atakabidhi chama kwa Rais Dk. John Magufuli.