23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

KAMATA KOLABO 5 ZILIZOMBAMBA 2017

NA CHRISTOPHER MSEKENA


 


KAZI kubwa imefanyika kwenye tasnia ya muziki mwaka huu, wasanii wake wameachia ngoma nyingi zilizotikisa chati za ndani na nje ya Bongo huku zikiweka rekodi kadha wa kadha.

Hapa nakusogezea nyimbo tano za kushirikiana (Kolabo) zilizofanya vizuri mwaka huu hata wewe pia msomaji wangu unaweza kunijuza kolabo zako bora zilizokubamba mwaka 2017.

Harmonize & Rich Mavoko

Ngoma inaitwa Show Me,  ni wimbo uliotoka Aprili 16 mwaka huu ukiwakutanisha wasanii wa lebo moja ya WCB. Huu ni wimbo wenye mahadhi yanayochezeka, ulijizolea umaarufu kwenye majumba ya starehe pamoja na mtandao wa YouTube ulifanya vizuri kwa kutazamwa na watu milioni 5.3 mpaka sasa.

ROSTAM

Hivi Ama Vile, ni kobalo iliyozalishwa na umoja marapa wakali Bongo, Roma Mkatoriki pamoja na Stamina ukiwa ni wimbo wao wa kwanza kama ROSTAM.

Kobabo hii ilitoka Agosti 18 mwaka huu kupokewa vyema na mashabiki kiasi kuwa wimbo bora kwenye shoo zote za Fiesta mwaka huu ambazo ROSTAM, walitumbuiza. Umoja huo hivi sasa unafanya vyema na ngoma yao mpya inayoitwa Kima_100.

Zilipendwa

Huu ni wimbo ambao upo kwenye orodha ya nyimbo anazosikiliza Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe. Ni ngoma iliyoimbwa kwa pamoja na wasanii wa lebo ya WCB, Diamond Platnumz, Rayvanny, Harmonize, Rich Mavoko, Queen Darleen, Lavalava na Maromboso.

Wimbo ulijizolea umaarufu Agosti 25 mwaka huu baada ya kutoka kipindi ambacho, ngoma ya Ali Kiba, Seduce Me ilikuwa inatamba hivyo Zilipendwa na Seduce Me zilikuwa zilichuana vikali na hakika zinastahili kuwa nyimbo kali kuwahi kutokea mwaka 2017.

Diamond Ft Morgan Heritage

Wimbo unaitwa Hallelujah, uliachiwa Sepetemba 28 mwaka huu na kuweka rekodi ya kipekee Afrika Mashariki na Kati kwa kutazamwa na watu zaidi ya milioni 1 ndani ya saa 16, na hivi sasa umetimiza miezi miwili tayari video yake iliyofanyika Uingereza imetazamwa na watu milioni 7.9.

Bila shaka hii ndiyo kolabo bora zaidi mwaka huu kwa Diamond ukiacha wimbo wake mpya wa Waka Waka aliomshirikisha Rick Ross ambao nao unazidi kufanya vizuri kwenye maduka ya kimtandao yanayouza nyimbo.

Abdul Kiba Ft Ali Kiba

Wimbo wao unaitwa Single, ni kazi mpya kutoka kwa Abdu Kiba akimshirikisha kaka yake, Ali Kiba. Ngoma hii imetoka Novemba 29 mwaka huu na kufanya vizuri kwenye mtandao wa YouTube na mtaani.

Siku moja baada ya kutoka wimbo huu, uliweza kuingia kwenye nafasi ya kwanza ya video zinazo-trendi na kuuondoa wimbo wa Sikomi wa Diamond Platnumz uliokuwa umesikilia nafasi hiyo kwa siku nne.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles