24.8 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Kamata kamata yaja kwa abiria wanaotupa taka ovyo

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam inatarajia kufanya operesheni ya kuwakamata watumiaji wa vyombo vya usafiri wanaotupa taka ovyo.

Akizungumza wakati wa usafi wa pamoja wa mwisho wa mwezi uliofanyika katika Kata ya Vingunguti, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Ng’wilabuzu Ludigija, amesema itahusisha pia kukagua vyombo vya usafiri ili kujiridhisha kama vina vifaa vya kutunzia taka.

“Tutaweka vijana kwenye baadhi ya maeneo ambao watakuwa wakifuatilia vyombo vya moto kuhakikisha abiria hawatupi taka nje, na kama daladala halina chombo cha kuhifadhia taka itatozwa faini.

“Wilaya ya Ilala na Jiji la Dar es Salaam ndiyo uso wa nchi, wageni wanaingia kupitia uwanja wa ndege lakini kuna bandari hivyo, tunataka jiji letu liwe ni kielelezo cha nchi yetu watu wanapokuja waone namna lilivyo safi,” amesema Ludigija.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Ng’wilabuzu Ludigija, akishiriki kufanya usafi wa pamoja uliofanyika katika Kata ya Vingunguti.

Aidha amewaagiza maofisa afya wa kata kuhakikisha wanatimiza wajibu wao kwa kupita kwenye mitaa na kufanya ukaguzi wa mara kwa mara badala ya kusubiri mwisho wa mwezi na watakaokiuka wachukuliwe hatua za kisheria kulingana na kanuni ndogo za usafi wa mazingira.

Naye Mkuu wa Idara ya Mazingira na Udhibiti wa Taka Ngumu, Rajabu Ngoda, amewataka wananchi kufanya usafi kila siku kwenye mazingira yao ya nyumbani na nje sambamba na usafi wa jumla wa kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mtakuja, Sharifu Mbulu, amewashukuru wananchi kwa kuitikia wito wa kufanya usafi katika maeneo yao na kuwataka waendeleze jambo hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles