WASHINGTON, Marekani
MAKAMU wa Rais wa Marekani, Kamala Harris, amekuwa mwanamke wa kwanza kushika mamlaka ya urais ndani ya taifa hilo.
Madaraka ya urais yalikuwa chini ya Harris kwa dakika 85, wakati ‘bosi’ wake, Rais Joe Biden, alipokuwa kwenye utaratibu wake wa kawaida wa kufanyiwa vipimo vya afya.
Wakati huo huo, Katibu Mkuu wa Ikulu, Jen Psaki, amesema halikuwa jambo la kushangaza kwa Makamu wa Rais kukalia kwa muda kiti cha Rais kwani liko Kikatiba kama ilivyowahi kutokea wakati wa utawala wa Rais George Bush.
Katika hatua nyingine, ripoti ya daktari wa Rais Biden iliyokuja baadaye ilieleza kuwa kiongozi huyo yuko vizuri na afya yake haimzuii kuendelea na majukumu yake.