30.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

KAKUNDA ATAKA HALMASHAURI KUKAMILISHA MPANGO KAZI WA ARDHI

 

|Hadija Omary, Lindi



Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Joseph Kakunda amewataka watendaji wote wa halmashauri nchini kukamilisha mipango ya matumizi bora ya ardhi kwa kila kijiji nchini ili wakulima, wafugaji na wavuvi wafanye shuguli zao bila migogoro baina yao.

Kakunda ameyasema hayo jana katika kilele cha maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima Nane Nane Kanda ya Kusini mwaka 2018 katika Viwanja vya Ngongo Manispaa ya Lindi.

“Kuna umuhimu wa kuongeza bidii katika kutunza mazingira ili kuwa na kilimo, mifugo na uvuvi endelevu bila kuzuka migogoro baina ya wakulima na wavuvi.

“Lakini pia nasisitiza juu ya kuwepo kwa ushirikiano kati ya serikali na wananchi katika kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji ili mfugaji apate eneo la kufuga na maji ya kunyweshea mifugo yake na wakati huo huo wakulima wanapata eneo la kulima bila kuingiliwa na mifugo itakayoharibu mazao yake,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles