26.7 C
Dar es Salaam
Monday, June 24, 2024

Contact us: [email protected]

Kairuki amuagiza RC Pwani kufuatilia ufunishaji kwa walimu

Na Gustafu Haule,Pwani

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Angela Kairuki amemwagiza Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakari Kunenge pamoja na Wakuu wa Wilaya kuhakikisha wanafuatilia ufundishaji wa walimu ili kuweza kuboresha elimu .

Pamoja na hilo amewataka viongozi hao kushughulikia changamoto na kero za walimu hususan katika kuwalipa stahiki zao ikiwemo fedha za malimbizo ya mishahara na madeni mbalimba ili waweze kufanya kazi zao kwa umahiri .

Waziri Kairuki ametoa maagizo hayo Januri 10, 2023 katika kikao kazi cha mapitio ya tathimini ya utekelezaji wa shughuli za uboreshaji na usimamizi wa elimu kwa mwaka 2022 na mpango wa mwaka 2023 kilichofanyika katika viwanja vya Shirika la Elimu Kibaha.

Katika kikao hicho kilichowakutanisha maafisa mbalimbali wa elimu kutoka wilaya zote za Mkoa wa Pwani, Wakurugenzi wa Halmashauri, maafisa elimu Kata, wakuu wa shule na viongozi wengine kilikuwa na lengo la kukumbushana namna ya kuboresha elimu ya Msingi na Sekondari.

Kairuki, alisema kuwa Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan imefanyakazi kubwa katika kuboresha mazingira ya ufundishaji kwa walimu na  hata kutatua changamoto nyingine.

Aidha, Kairuki amemshukuru Rais Dk. Samia kwa jitihada hizo maana angeweza kuingia madarakani na kufuta mpango wa elimu bure lakini cha ajabu katika kipindi kifupi cha Novemba 2021 na Desimba 2022 ameendeleza  zaidi mpango huo na kuweza kujenga madarasa 2,3000 .

Kairuki, ameongeza kuwa pamoja nakujenga madarasa hayo lakini bado ameendelea kutoa fedha nyingi kwa ajili ya kujenga Shule mpya katika Mikoa mbalimbali hapa nchini zikiwemo Shule za Sekondari za wasichana.

“Tumeona jinsi ambavyo Rais wetu anavyofanyakazi hususani katika sekta hii ya elimu kwahiyo niwaombe tuendelee kuyasemea mafanikio haya ili kuweza kumtia moyo Mheshimiwa Rais kwa kazi kubwa anayofanya,”alisema Kairuki.

Kairuki pamoja na mafanikio makubwa yaliyopo lakini bado zipo changamoto mbalimbali ikiwemo watoto wa awali kushindwa kusoma na kuandika ,pamoja na wanafunzi wanaoingia kidato cha kwanza kushindwa kuongea lugha ya kiingereza.

Alisema,sio changamoto hiyo tu lakini kuna sababu za kimila na desturi pamoja na utoro zinazosababisha watoto kushindwa kufikia malengo na kwamba amewataka maafisa hao kubuni mikakati sahihi ya kuthibiti changamoto hizo.

“Lazima tuwe na jitihada za makusudi za kuboresha elimu ya Msingi na Sekondari lakini baada ya mikakati hiyo hatutaishia hapo kwani tutaendelea kufanya tathmini na ikiwezekana mwaka ujao tutakuja kutoa tunzo kwa walimu na shule zitakazofanya vizuri,” alisema Kairuki

Mbali na kikao hicho lakini pia Kairuki akiwa Mkoani Pwani alitembelea na kukagua Shule ya Sekondari Sofu pamoja na Shule ya Sekondari Bundikani zilizopo Mjini Kibaha na kufuruhishwa na ujenzi huo huku akiwataka walimu kusimamia vyema miundombinu ya Shule hizo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakari Kunenge,alisema kuwa tayari Mkoa ulishafanya kikao kama hicho na utekelezaji wake umekwenda vizuri.

Kunenge,alisema kuwa walifanya tathmini na kubaini Mkoa wa Pwani Kuna Mila na desturi na tathmini hiyo ilikuwa pamoja na kuwauliza wanafunzi kama Kuna utaratibu wa masomo wanapofika nyumbani,vitabu na vifaa vingine vya kujisomea.

Aidha, Kunenge amempongeza Rais wa awamu ya Sita Dk. Samia kwa kazi kubwa anayoifanya hasa katika kutambua masuala mbalimbali ya elimu yaliyopo Mkoani Pwani.

Hatahivyo, Mkurugenzi wa elimu (Tamisemi), Vicent Kayombo alisema kuwa bado kuna changamoto ya wanafunzi kutokujua kusoma na kuandika na kuhesabu lakini changamoto hizo zinaendelea kufanyiwa kazi ili kusudi ifikapo 2024 ziwe zimekwisha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles