25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yatoa msaada kwa waathirika wa mafuriko Mbeya

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Serikali upitia Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu imetoa msaada kwa wananchi walioathirika na mafuriko ya maji mkoani Mbeya, yaliyosabisha nyumba kubomoka, kuharibika kwa vifaa, vyakula, uharibifu wa mifugo na mazao yaliyoko shambani.

Msaada huo ni magodoro 300 kwa kuanzia, mablanketi 1,200 ya wakubwa na wadogo, mikeka 600, madumu ya maji, sufuria bakuli sahani na vijiko kwa kila familia ambayo imeathirika.

Msaada huo umekabidhiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, George Simbachawene alipotembelea maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko hayo katika kata saba mkoani Mbeya kutokana na mvua kubwa iliyonyesha Januari 7, mwaka huu,

“Kwa mujibu wa sheria no. 6 ya Maafa ya Mwaka 2022 sisi Ofisi ya Waziri Mkuu tunayo dhamana ya kuwaunganisha wadau ili kuwasaidia watu walioathirika na tutafanya hivyo kwa kutumia ofisi zetu za mkoa na wilaya, naomba wadau wote wa ndani na nje ya mkoa wa Mbeya kutusaidia ili kuhakikisha watu hawa wanarudi katika hali yao.,” amesema Simbachawene na kuongeza:

“Natoa pole kwa wote walioathirika, TARURA kwa kushirikiana TANROAD Halmashauri ya Jiji la Mbeya na Halmashauri ya Mbeya vijijini wahakikishe wanaenda kuona kwenye vyanzo kuangalia ni eneo gani maji yametoka kwenye mkondo wake wa asili,” amesema.

Awali, Mbunge wa Mbeya Mjiniambaye pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson ameishukuru Serikali kwa mchango iliyoutoa kwa waathirika wa mafuriko hayop mkoani humo huku akitoa angalizo kwa halmashauri.

“Naomba sisi kama halmashauri tusitoe vibali vya ujenzi kwenye  maeneo ambayo ni mikondo ya maji, kwa sababu athari za mafuriko zinarudisha nyuma maendeleo ya uchumi kwa wananchi,” amesema Dk. Tulia.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera katika taarifa yake amesema watu waliopata athari za mafuriko ya maji ni kaya 281 zenye idadi ya watu 1,405 ambao wanahitaji chakula takribani tani 50 kwa miezi mitatu ili ziweze kuwasaidia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles