26.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 21, 2024

Contact us: [email protected]

Kahatano: Faini za papo hapo barabarani utata

Johansen Kahatano
Ofisa Mnadhimu wa kikosi cha Usalama Barabarani (SACP), Johansen Kahatano

Na Hadia Khamis, Dar es Salaam

KIKOSI cha Usalama Barabarani nchini kimekiri kuwapo udhaifu katika utaratibu wa ulipaji faini za papo kwa papo kwa madereva wanaokamatwa na makosa.

Ofisa Mnadhimu wa kikosi cha Usalama Barabarani (SACP), Johansen Kahatano, alisema hayo katika mahojiano maalumu na MTANZANIA Jumamosi juu ya malalamiko yanayotolewa na wananchi kuhusiana na ulipaji faini kwa makosa ya usalama barabarani kwamba fedha hizo zinaishia mikononi mwa askari hao.

Baadhi ya wananchi walidai askari wa kikosi hicho hujitengenezea hadi Sh milioni moja kwa siku ikiwa ni fedha zao binafsi bila ya Jeshi la Polisi kujua hilo.

“Askari wa usalama barabarani ni miongoni mwa watu wenye utajiri wa kutisha na kumiliki mali nyingi kuliko watu wengine, ambapo kwa siku moja anaweza kujiingizia hadi laki saba,” alisema mmoja wa raia aliyekataa kutajwa jina lake gazetini.

Baadhi ya madereva waliohojiwa wameainisha maelezo ya fomu ya makosa ya usalama barabarani kifungu namba mbili ambacho humtaka dereva anayepatikana na kosa kulipa faini ndani ya siku saba na sio papo kwa papo.

“Kama mimi ni dereva nimekamatwa na kosa na nimelipa faini ya papo kwa papo, kwanini askari asinipe risiti inayoonesha uhalali wa malipo yangu niliyolipa badala yake ananipa karatasi ya notification peke yake.

Nina mashaka na hizi fedha kama hazifiki sehemu inayotakiwa, kwa sababu hakuna kielelezo kinachonifanya nijiridhishe kama hizo fedha zinafika kweli,” alisema mmoja wa madereva aliyekamatwa na askari wa kikosi cha usalama barabarani.

Alisema kitendo cha askari wa usalama barabarani kuandika makosa hayo na kushinikiza madereva wakalipe faini kituoni huku wanazuia leseni ili waone usumbufu na kukubali kulipa faini ya papo kwa papo si cha sheria.

Akijibu tuhuma hizo, Kahatano alisema kitengo cha usalama barabarani kimeandaa mkakati wa kulipa faini kwa njia ya mtandao kama ilivyo kwa nchi za jirani ili kuondoa usumbufu wa kuandika faini za papo kwa papo.

“Ulipaji faini papo kwa papo umekuwa ukilalamikiwa na watu wengi, hivyo kama Jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani tunatarajia kuanzisha mfumo wa ulipaji faini kwa njia ya akaunti au kwa njia ya simu kama zinavyotolewa huduma za selcom,” alisema Kahatano.

Alisema kwa mujibu wa sheria ya makosa ya usalama barabarani, askari anapomkamata mtu kwa kosa lolote lazima amwambie kosa lake na ndipo amuandikie kosa hilo iwapo kama atakubali.

Kahatano alisema mkosaji anapokubali kosa lake anatakiwa kulipa faini ndani ya siku saba huku akiwa chini ya dhamana ikiwa ni pamoja na kuacha leseni yake kwa askari au kudhaminiwa na askari anayemtambua.

“Tatizo linakuja pale ambapo mtu atalipa faini bila ya kupewa risiti anashindwa kuamini kwamba zile fedha zinafika katika kituo cha polisi na ukweli ni kwamba, risiti zinakuwapo kwa mhasibu wa kituo na sio kwa askari.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles