Kagasheki amkumbuka Samuel Sitta

0
803

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Waziri wa zamani wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki amemkumbuka aliyekuwa Spika wa Bunge, marehemu Samuel Sitta.

Kagasheki katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter, ameelezea namna anavyomkumbuka Sitta kwa namna alivyokuwa akitenda kazi katika bunge hilo.

“Siku ya leo, mwaka 2016 alitutoka Mzee Samuel Sitta. Tukimwita, Mzee wa viwango na spidi. Hakika katika uongozi wake kama Spika, Bunge la JMT lilipitia mabadiliko makubwa sana.

Atakumbukwa kwa mchango wake ndani na nje ya Bunge. Rest In Peace my dear senior brother,” ameandika Balozi Kagasheki.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here