27.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, August 17, 2022

Mwanafunzi asiyeona abakwa na walimu wake India

India

Walimu wawili nchini India, wanatuhumiwa kumbaka msichana kipofu aliyekuwa akisoma katika shule ya watoto wenye ulemavu kwa muda wa miezi miwili.

Walimu hao Chaman Thakor, (62) na Jayanti Thakor (30), inadaiwa walimbaka msichana huyo wa miaka 15 kwenye chumba cha muziki cha shule hiyo.

Taarifa ya shambulio hilo ilibainika baada ya familia ya mwanafunzi huyo kukataa kurudi shule ya bweni huko Ambaji, Gujarat baada ya likizo ya Diwali mwezi uliopita.

Mwanafunzi huyo alivunjika moyo na kumwambia shangazi yake, akielezea shida anazopata mikononi mwa walimu hao wawili ambapo shangazi yake huyo aliwasiliana na polisi na kuwaelezea.

Aliwaambia alibakwa kwanza kwenye chumba cha muziki na Chaman Thakor miezi miwili iliyopita na kisha Jayanthi Thakor alidaiwa kumshambulia katika chumba kimoja siku tatu baadaye.

Msichana alikuwa ameandikishwa katika shule ya bweni Julai mwaka huu kusoma muziki na alikuwa akisoma darasa la nane katika kijiji chake.

Inspekta wa polisi, Ambaji, JB Agrawat, aliliambia gazeti la Times la India kwamba watu hao wawili walikimbia baada ya uhalifu wao kugunduliwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,903FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles