24.4 C
Dar es Salaam
Thursday, October 31, 2024

Contact us: [email protected]

Kagame amfukuza waziri wa afya

RAIS wa Rwanda, Paul Kagame
RAIS wa Rwanda, Paul Kagame

KIGALI, RWANDA

RAIS wa Rwanda, Paul Kagame, amemtimua waziri wake wa afya, Dk. Agnes Binagwaho, aliyeongoza wizara hiyo kwa miaka mitano.

Tangazo lililotiwa saini na Waziri Mkuu, Anastase Murekezi, limebainisha kuwa Rais Kagame katika mamlaka yake amemfuta kazi waziri huyo bila kutoa maelezo zaidi.

Lakini wadadisi wanasema kutimuliwa kwake huenda kumetokana na utendaji kazi usioridhisha na matatizo yanayoikumba wizara hiyo kwa sasa.

Wakati wa mkutano wa kitaifa Desemba mwaka jana, waziri huyo alikosolewa vikali na washiriki, waliobainisha tatizo kubwa la ugonjwa wa malaria.

Takwimu zilizopo wizarani zinabainisha kuwa watu zaidi ya milioni 2.5 waliathirika na ugonjwa huo mwaka jana.

Hata hivyo, kipindi cha miezi sita pekee ya mwaka huu kulikuwa na wagonjwa milioni 1.4, idadi ambayo ni kubwa ikilinganishwa na miaka mitano iliyopita, Rwanda ilipokuwa miongoni mwa mataifa yaliyokuwa katika nafasi nzuri ya kuutokomeza ugonjwa huo.

Tatizo lililobainishwa na wakosoaji ni uzembe uliofanywa na Wizara ya Afya kuagiza vyandarua visivyokidhi viwango vya ubora, ambavyo viliigharimu dola milioni 15.

Katika ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Mali ya Umma, wizara hiyo ilibainisha pengo la dola milioni 10 zilizotoweka.

Kadhalika kuna suala la utendaji kazi mbovu katika hospitali za Serikali, ambako madaktari bingwa wanazikimbia kutokana na udogo wa mishahara na kujiunga na hospitali binafsi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles