26.9 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Kafulila: Tanzania tunatakiwa kuliongoza Bara la Afrika

Na Derick Milton, Simiyu

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, David Kafulila amesema Tanzania inatakiwa kuliongoza Bara zima la Afrika, kwani wakati wa ukoloni mataifa mengi ya Afrika yalikombolewa kupitia Tanzania.

Amesema kuwa wakati huo Tanzania ndicho kilikuwa kituo cha ukombozi wa mataifa mengi ya Afrika kutoka kwa wakoloni, ambapo Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julias Nyerere ndiye aliongoza harakati hizo.

Mkuu huyo wa Mkoa emesema hayo leo, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mashujaa ambayo kimkoa imefanyika katika mnara wa mashujaa ulioko kwenye ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi.

“Maazimisho ya siku ya mashujaa, lazima kama vijana na viongozi yatukumbushe nafasi ya Taifa letu katika Bara la Afrika iko wapi? Lazima tulipiganie taifa letu tena liwe kiongozi katika bara hili.

“Utakuwa kijana wa ajabu usipojua historia ya taifa lako, ni sisi tena Tanzania tunatakiwa kuliongoza bara letu la Afrika, ili kufanikisha haya kila kijana, kila kiongozi atimize wajibu wake kwenye eneo lake na kuwa mzalendo wa kweli,” amesema Kafulila.

Amesema kuwa wazee ambao walipigana vita wakati wa mkoloni, walitimiza wajibu kila mtu kwenye eneo lake, lakini pia walitanguliza uzalendo mbele ndiyo maana waliifanya Tanzania kuwa kituo cha ukombozi wa Afrika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles