30.1 C
Dar es Salaam
Saturday, June 15, 2024

Contact us: [email protected]

Kaduma amchambua Rais Magufuli

Ibrahim Kaduma
Ibrahim Kaduma

Na Jonas Mushi, Dar es Salaam

ALIYEWAHI kuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM) na Waziri wa Mambo ya Nje, Ibrahim Kaduma  amesema kasi ya Rais Dk.John Magufuli  inaweza kuirudisha nchi katika misingi iliyoasisiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere.

Hayo aliyasema   Dar es Salaam jana alipozungumza   na MTANZANIA katikaTtamasha la nane la Kigoda cha Mwalimu Nyerere kuhusu jinsi viongozi wa sasa wanavyoendeleza misingi iliyoanzishwa Rais huyo wa kwanza wa Tanzania.

Alisema tangu Nyerere aondoke madarakani suala la maadili ya uongozi lilitetereka huku viongozi wakijinufaisha   badala ya kuleta maendeleo kwa wananchi wao.

“Tangu Mwalimu aondoke madarakani baadhi ya misingi ikiwamo ya maadili na maendeleo ya watu imetetereka kwa kiasi kikubwa,” alisema na kuongeza:

“Tunaweza kuwa na matumaini na Rais Magufuli kama ataendelea na kasi yake anaweza kuturudisha kule kwa Mwalimu Nyerere”.

Alisema Rais Magufuli ameanza kuonyesha njia ya kuelekea kusimamia maadili ya viongozi   na kufungamanisha maendeleo na watu.

Ni vema rais aweke wazi dira yake na aijengee misingi ya  sheria ili kila mwananchi ajue serikali inataka kujenga nchi ya aina gani, alisema.

Awali akiwasilisha mada katika tamasha hilo iliyohusu “Mwalimu Nyerere na Uongozi” Kaduma alisema uongozi kwa Mwalimu haukua fedha na ufahari bali kujituma na kujitoa kwa ajili ya watu.

Kaduma alisema kiongozi anatakiwa asiwe mbinafsi bali awe tayari kuacha hata maslahi yake kwa ajili ya maslahi ya umma.

Dk. Bakari

Akizungumzia mpango wa serikali wa kugawa Sh milioni 50 kila kijiji, aliyekuwa Mkuu wa Chuo cha Sanaa cha Bagamoyo (TaSuBA) na mmoja wa waliokuwa Mameneja wa vijiji vya ujamaa, Dk. Juma Bakari alisema mpango huo unaweza usifanikiwe kutokana na kutokuwa na maandalizi mazuri.

Akieleza suala hilo kwa uzoefu wa vijiji vya ujamaa, alisema serikali ya Mwalimu Nyerere haikuwa na maandalizi ya mpango ule ndiyo maana haukufanikiwa na baadaye ukafa.

Suala la Sh milioni 50 kila kijiji halikuwa wazo la wananchi bali ni wazo la mtu mmoja na hivyo linaweza lisitatue changamoto za watu wa vijijini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles