27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 13, 2024

Contact us: [email protected]

Kaduguda ‘apasuka’ suala la Mo Simba

kadugudaNA ADAM MKWEPU, DAR ES SALAAM

KATIBU Mkuu wa zamani wa klabu ya Simba, Mwina Kaduguda, ameeleza kuwa klabu hiyo kwa sasa haihitaji mtu mwenye fedha ili kuimiliki badala yake inahitaji mwenye uwezo wa kufikiri na kutumia fursa ya rasilimali zilizopo ndani ya klabu hiyo ili kupata fedha.

Hatua hiyo imekuja baada ya kuwepo kwa mjadala mkali uliokuwa ukimhusu mfanyabiashara maarufu nchini, Mohammed Dewji ‘Mo’, kutaka kuwekeza Sh bilioni 20 katika klabu hiyo.

Akizungumza katika kituo kimoja cha redio nchini, Kaduguda alisema klabu hiyo inashindwa kujua cha kufanya kwa sababu uongozi uliopo ni wavivu wa kufikiri ili kuona fursa zilizopo.

“Uswahili ndio unaiponza klabu hii kutoendelea, kama tukiwa vizuri na viongozi wakaacha uvivu wa kufikiri Simba inaweza kufika mbali,” alisema Kaduguda.

Alisema kwa muda ambao klabu hiyo imeanzishwa pamoja na miradi iliyopo, haina haja ya kuwa na mmiliki ili kuifadhili kwa fedha badala yake wanapaswa kutumia akili na maarifa ili kutumia fursa.

“Simba haina mipango kwa kuwa tatizo walilonalo ni fedha na si mtu mwenye fedha, hata hivyo thamani yake si shilingi bilioni 20 kama  inavyodaiwa na huyo mtu anayetaka kuwekeza ingawa mimi kwangu naona kama propaganda tu.

“Nilitarajia huyo mtu angezungumza  na uongozi wa Simba mazungumzo ya awali kisha aje na maelekezo yenye mchanganuo juu ya hilo, lakini hapa naona kuna ushawishi wa wanachama ndani yake,” alisema Kaduguda.

Kaduguda alidai kwamba, hakuna shabiki na mpenzi wa klabu hiyo asiyependa kuona maendeleo na kuongeza kwamba, kuchukuliwa na tajiri huyo si suluhisho la matatizo ya klabu hiyo.

“Kuna tofauti kati ya ufadhili na udhamini, ufadhili ni hisani haina tofauti na huruma ya mtu wakati udhamini unatokana na utaratibu wa kisheria ambao mimi kipindi cha uongozi wangu tulifanikiwa kuwa nao.

“Simba wana wadhamini aina nne tofauti ambao ni TBL, Push Mobile, Vodacom pamoja na kampuni ya vifaa vya michezo ya Marekani, lakini kinachotokea kwa viongozi wanadai kwamba kuna wafadhili wawili tu huku wakificha wengine,” alisisitiza Kaduguda.

Alisema kwamba kutokana na ufadhili huo klabu hiyo ina uwezo wa kuingiza Sh bilioni 2 kwa mwezi na kuifanya kutohitaji tajiri yeyote ili ifanye shughuli zake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles