23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

TGNP walia na uteuzi wa Rais Magufuli

lilianNa Veronica Romwald, Dar es Salaam

MTANDAO wa Wanawake wa Katiba na Uchaguzi, umemwomba Rais Dk. John Magufuli, kusimamia  kikamilifu  utekelezwaji  wa  mikataba  mbalimbali iliyosainiwa  na  Tanzania  hasa  ile  ya  usawa  wa  kijinsia  ili kupunguza  pengo  lililopo kuelekea usawa  wa  50/50  katika  nafasi  za  uongozi.

Mikataba  hiyo  ni  pamoja  na  Mpango  Kazi  wa  Beijing  (1995), Mkataba  wa  Maputo,  Mkataba  wa  Nyongeza  wa  Jinsia  na  Maendeleo  Kusini  mwa  Afrika  (SADC  Gender Protocol)  na  Tamko  la  Umoja  wa  Mataifa  la  Haki  za  Binaadamu  la mwaka 1948.

Rai hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP-Mtandao, Lilian Liundi katika taarifa yake aliyotumwa kwa vyombo vya habari, ambapo alisema hiyo ni kwa sababu kumekuwapo na idadi ndogo ya wanawake wanaoteuliwa kuliko ile ya wanaume katika ngazi ya maamuzi.

“Tumefuatilia tangu wakati wa uchaguzi na wakati wa   uteuzi  wa  mawaziri, makatibu wakuu, manaibu na   wakuu wa  idara na taasisi mbalimbali  uliofanywa  hivi  karibuni na Rais Magufuli.

“Katika  uteuzi huo kuna jumla  ya  makatibu  wakuu na  manaibu katibu wakuu  50  idadi ambayo  ni  pungufu  kidogo  ikilinganishwa  na  mwaka  2014  ambapo walikuwa  53,” alisema.

Alisema idadi  ya makatibu  wakuu  imeongezeka  kutoka  23  mwaka  2014  hadi  29  wakati  manaibu  katibu  wakuu  imepungua kutoka  30  mwaka  2014  hadi  21  mwaka  huu.

Alisema hata hivyo kati  ya  nafasi  zote  50  za  walioteuliwa    wanawake wapo 10 tu idadi ambayo ni sawa  na  asilimia 20 ikilinganishwa na wanaume ambao ni asilimia 80.

Alisema idadi  ya  makatibu  wakuu  na  manaibu katibu  wakuu  wanawake  imepungua  kwa  kiasi  kikubwa ambapo takwimu  za  mwaka  2014  zinaonesha  walikuwa  20 sawa  na  asilimia  37.7 huku wanaume  wakiwa  33  sawa  na  asilimia  62.3.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles