29.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

KABUDI: UKOSEFU VYETI VYA KUZALIWA UMEIKOSESHA SERIKALI TAARIFA

WAZIRI wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi

 

 

Na RAMADHAN HASSAN-DODOMA

WAZIRI wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi, amesema asilimia 13.4 ya Watanzania ndio wamesajiliwa na kupewa vyeti vya kuzaliwa.

Amesema kutokana na kuwapo idadi hiyo ndogo, kunasababisha Serikali kukosa taarifa muhimu ambazo zingesaidia kupanga mipango mbalimbali.

Profesa Kabudi alisema hayo mjini hapa jana wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mapitio ya mfumo wa sheria zinazohusu usajili wa matukio muhimu ya binadamu Tanzania Bara.

“Kumbukumbu za matukio hayo ya kuwa na vyeti vya kuzaliwa ni takwimu za sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012, ambazo zinaonyesha asilimia 13.4 tu ya Watanzania ndio wamesajiliwa na kupewa vyeti vya kuzaliwa,’’ alisema.

Alisema changamoto kubwa katika upatikanaji wa vyeti vya kuzaliwa ni   kutokana na mfumo huo kutokuwa rafiki, hasa kwa watu wanaoishi vijijini.

 “Walio wengi hasa wa maeneo ya vijijini wanatakiwa kufuata huduma ya usajili makao makuu ya wilaya, kwa sababu ngazi ya chini ya usajili ni ofisi ya katibu tawala wa wilaya, hii imekuwa ni changamoto kubwa,’’ alisema.

Pia alisema Serikali iliona kuna haja ya kuikabidhi Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania jukumu la kupitia mfumo wa sheria unaohusu matukio muhimu ya binadamu kwa madhumuni ya kupendekeza mfumo wa usajili ili kuongeza ufanisi na tija.

“Usajili wa matukio muhimu ya binadamu ni hatua muhimu katika kuwezesha watoto kupata haki za msingi za mtu kama vile kupata jina, kuwatambua wazazi wa mtoto na uraia,’’ alisema.

Alisema usajili humuwezesha mtu kupata haki za msingi kama vile haki ya kupata huduma ya afya, elimu, kupiga kura, kuchaguliwa na kupata kazi.

Pia alisema usajili hutoa kinga kwa watoto dhidi ya dhuluma na manyanyaso kama vile ajira za watoto wadogo na kushtakiwa kijinai kama watu wazima.

“Kila mmoja wenu atambue kwamba sheria itakayotungwa kutokana na maoni na ushauri mnaoutoa, itatuhusu sisi wote, watoto na ndugu zetu na taifa kwa ujumla,’’ alisema.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria, Jaji Aloysius Mujulizi, alisema Serikali imekuwa ikichukua hatua mbalimbali za kuhakikisha mfumo wa usajili unakuwa rafiki, madhubuti na unaozingatia maendeleo ya kijamii, kisiasa, kiuchumi na teknolojia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles