24.4 C
Dar es Salaam
Thursday, October 31, 2024

Contact us: [email protected]

JWTZ wafanya usafi Dar

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Na WAANDISHI WETU,

JESHI la Wananchi Tanzania (JWTZ) limefanya maadhimisho ya kutimiza miaka 52 tangu kuanzishwa kwake kwa kufanya shughuli mbalimbali za jamii ikiwamo kufanya usafi na kuchangia damu.

Shughuli hizo zilianza tangu Septemba 25 mwaka huu na kufikia kilele chake jana ambako kwa upande wa Dar es Salaam wanajeshi walishiriki katika kufanya usafi katika maeneo yao na kuchangia damu katika vituo vya afya.

Pia jeshi hilo lilipamba maadhimishio hayo kwa kurusha angani ndege za vita ambazo zilipita kwa kasi na katika anga la chini kwa staili mbalimbali kwa   zaidi ya saa moja.

Akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea kambi ya Jeshi ya Lugalo wilayani Kinondoni, Kamanda wa Brigedia ya Mashariki (Brigedia ya Chui), Brigedia Generali Sharif Othman, alitoa wito kwa jamii nzima kudumisha suala la usafi  kuepuka magonjwa.

Alisema suala la usafi ni utamaduni wa jeshi hilo kwa vile  limekuwa mfano katika utunzaji wa mazingira yake hivyo limeamua kufanya katika mitaa   kutoa hamasa kwa jamii nzima kuwa na tabia ya kufanya usafi.

“Usafi ni utamaduni wetu kwa sababu huwa tunapata mafunzo ya utunzaji wa mazingira kuanzia ngazi ya askari hadi maofisa,” alisema Othman na kuongeza:

“Unapojiweka katika mazingira ya usafi, ukafanya mazoezi na kuzingatia ulaji mzuri wa chakula basi unajiepusha na magonjwa mengi hivyo tunatoa wito kwa jamii kuiga mambo haya.

“Tulianza maadhimishi tangu Septemba 25 mwaka huu kwa kufanya usafi ndani ya kambi zetu na nje ya kambi, kuchangia damu na madaktari wetu wakatoa huduma za afya kwa jamii”.

Pia alisema mapema asubuhi jana walitembelewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi na wajumbe wa Kamati ya Amani ya Mkoa Dar es Salaam na kuungana nao katika shughuli hizo.

Alisema jana katika kilele cha maadhimisho hayo, walisheherekea kwa kufanya usafi ndani ya kambi yao na kuchangia damu katika vituo mbalimbali vya afya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles