Justin Bieber ateguka mguu

Justin Bieber
Justin Bieber
Justin Bieber

NEW YORK, MAREKANI

MSANII wa muziki wa Pop nchini Canada, Justin Bieber, ameteguka mguu wa kushoto wakati akifanya mazoezi ya kucheza mchezo wa kikapu kwenye Uwanja wa Bank Arena.

Nyota huyo aliumia baada ya kuanguka wakati anapachika kikapu na kuufanya mguu uvimbe kabla ya kukimbizwa hospitali. Hata hivyo inadaiwa kwamba hali yake inaendelea vizuri baada ya kupata matibabu.

Kupitia akaunti yake ya Instagram, msanii huyo aliweka picha akionyesha mguu huo jinsi ulivyovimba, lakini amewatoa wasi wasi mashabiki wake.

“Ninaendelea vizuri kwa sasa na naweza kutembea, lakini awali hali hiyo ilinitisha sana kwa kuwa nilijua kama nimevunjika, nawapenda sana,” aliandika Bieber.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here