23.5 C
Dar es Salaam
Monday, June 24, 2024

Contact us: [email protected]

Black Coffee ashinda tuzo BET

black coffee
black coffee

LOS ANGELES, MAREKANI

PRODYUZA, DJ na mwimbaji mwenye mafanikio makubwa katika muziki nchini Afrika Kusini, Black Coffee, amenyakua tuzo ya Black Entertainment Television (BET), kipengele cha msanii bora wa kimataifa kutoka Afrika ‘Best International Act – Africa’ iliyokuwa ikiwaniwa na wasanii wengine saba kutoka Afrika akiwemo Nasib Abdul wa Tanzania.

Wasanii wengine waliowashindanishwa na Black Coffee katika tuzo hiyo ni pamoja na wenzake wawili kutoka nchini Afrika Kusini, Cassper Nyovest na Kiernan Forbes ‘A.K.A’.

Wengine ni kutoka Nigeria, Wizkid na Yemi Alade kutoka Ivory Coast ni Serge Beynaud kutoka Ghana ni Vera Hamenoo na Nasibu Abdul (Diamond) kutoka Tanzania.

Baada ya kupokea tuzo hiyo iliyotolewa Los Angeles, Marekani, Black Coffee alisema angekuwa na furaha pia kama washiriki wenzake wawili wangeshinda badala yake.

“Yeyote angeshinda ningekuwa na furaha kama nilivyo sasa nimeshinda mimi lakini nina furaha kwa kuwa tulipata nafasi wasanii watatu kutoka Afrika Kusini nikiwemo mimi, AKA na Cassper Nyovest, hivyo tumeiwakilisha vyema Afrika Kusini,’’ alijieleza Black.

Msanii huyo amewashukuru mashabiki wake kwa kumpigia kura na kufanikiwa kutwaa tuzo hiyo, hata hivyo amedai kwamba tuzo hiyo ni kwa ajili ya mashabiki wote waliompigia kura.

“Asante Afrika, hii tuzo ni kwa ajili ya watu wangu wote,’’ aliandika katika ukurasa wake wa twitter.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles