28.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

JULIA GUNTHEL: MWANAMKE MNYUMBULIFU ALIYEITEKA DUNIA

Julia Gunthel
Julia Gunthel

JOSEPH HIZA Na MASHIRIKA,


 

WENGI wetu, kupinda na kugusa vidole vya miguu yetu kwa paji la uso kunaweza kuonekana kuwa kazi isiyowezekana.

Lakini kwa Julia Günthel, mwanamke mnyumbulifu kuliko wote duniani, ni suala dogo kama kupasha viungo tu.

Uwezo wa kushangaza wa Gunther anayejulikana zaidi kwa jina la utani la Zlata lenye maana ya mw

anamke wa dhahabu umekuwa ukioneshwa katika kipindi cha televisheni cha Discovery Channel nchini Ujerumani tangu mwaka 2010.

Madaktari waliuchunguza mwili wake kwa mashine ya MRI, ambao kwa mshangao wao walibaini kuwa kano zake (ligaments) zi sawa na zile za watoto wachanga.

Kwa kawaida kano hukomaa kwa kadiri umri unavyoongezeka na hivyo kupunguza hali ya unyumbulifu,  lakini kwa Zlata, anaweza kukaa mikao au maumbo, ambayo kwa wengi wetu tutakijaribu kuiga tutaishia kuvunjika mgongo.

Mzaliwa huyo wa Urusi anayeweza hujinyonga au kupinda katika maumbo mbalimbali, amevunja rekodi nyingi za dunia kwa unyumbulifu wake huo.

Mwanasarakasi huyo wa zamani, ambaye ana urefu wa futi tano na inchi nane, yu mnyumbulifu mno kiasi kuwa anaweza kuingia katika sanduku la urefu na upana wa sentimita 50.

Gunthel mwenye umri wa miaka 30 anasema; “Kukaa mikao yote hii huwa najisikia kawaida sana. Lakini wakati mwingine najisikia vibaya kidogo iwapo nitakaa katika mikao hiyo kwa muda mrefu kwa ajili ya kupiga picha.”

‘Lakini nadhani hii ni kawaida sawa na mtu yeyote ambaye akikaa mkao hata wa kawaida kwa muda mrefu misuli hukakamaa.’

Katika umri wa miaka minne, mwalimu wake wa shule ya awali alibaini namna alivyo mwepesi mno kupinda kwa mikao tofauti.

Baada ya kugundua hilo akawa akipenda kujipinda pinda katika maumbo na mikao tofauti ya kushangaza, akajiunga na darasa la sarakasi kabla ya kukigeuza kipaji chake kuwa kazi rasmi.

Alisema: ‘mara nilipoanza kufanya hii, nikawa nikipenda kuifanya kila mara na nikafahamu kuwa nitakuja ifanya kwa kipindi chote cha maisha yangu.”

Lakini daima utotoni haikuwa rahisi, wengi wa wanafunzi wenzake Zlata walikuwa na wivu na uwezo wake huo wa ajabu.

Anaeleza: ‘Nchini Urusi kuwa mnyumbulifu wa mwili ni kitu cha kawaida sana kwa sababu kila mmoja anaingia katika michezo ya sarakasi. Lakini baadhi ya wasichana hawakupenda namna nilivyokuwa mzuri zaidi kwa mchezo huo.

Akawa mwanasarakasi kipindi chote cha utoto wake na kazi kama mpinda viungo (contortionist) alipokuwa na umri wa miaka 10 tu.

Günthel akahamia Ujerumani na familia yake akiwa na umri wa miaka 16 anakoishi hadi sasa na ambako ndiko neno ‘Zlata’ lilikozaliwa.

Mara alipofika Ujerumani alianza kusomea Sanaa ya sarakasi.

Ni huko ndiko alikovunja rekodi ya dunia kwa kutumia nguvu ya mgongo wake na miguu kupinda na kuvunja maputo matatu kwa sekunde 12.

Zlata alisema alifanya kazi kwa bidii kwa kufanyia mazoezi kipaji chake hicho kila siku ili kuendeleza umbo na unyumbulifu wake.

Aliongeza: ‘Siupi kipaumbele mlo katika kuendeleza umbo na unyumbulifu bali mazoezi. Nafanya mazoezi kwa bidii ili kuiweka misuli yangu sawa na kuwa mnyumbulifu zaidi kwa kadiri iwezekanavyo.’

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles