30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

VYUO VITANO VINAVYOTAMBA KWA KILA BARA DUNIANI

Chuo kikuu cha Buenos Aires  CHA Argentina
Chuo kikuu cha Buenos Aires, Argentina

Na FARAJA MASINDE,


 

MWAKA 2016 tayari umekatika na sasa tuko kwenye mwaka mwingine je, vipi ushapata chuo utakachoenda kusoma mwaka huu? Kama bado hujajua uende ukasome chuo kipi na bara gani litakufaa, basi hujakosea kusoma safu hii.

Sasa hivi matangazo ya vyuo vikuu vya ng’ambo yamekuwa mengi huku kila tangazo likiwa na sifa kedekede kuhusu chuo fulani jambo ambalo huenda likawa linakuchanganya akili, mbaya zaidi matangazo haya kila moja limekuwa likinadi namna ambavyo wanaweza kukupa ufadhili wa masomo hadi asilimia 100.

Ni kweli inawezekana, kwani Waswahili wanasema; “kila mwamba ngoma huvutia kwake.” Jambo la kuzingatia iwapo unatafuta chuo bora hasa vyuo vya nje ya nchi ni lazima uhakikishe kwanza unapata chuo bora kitaaluma, lakini pia chenye jina kubwa kwa maana ya kinachoweza kutambulika kirahisi na kukupa kazi na kukusaidia kupata kazi kwa haraka zaidi.

Itakuwa haina maana kama utasoma nje ya nchi alafu uje uhangaike kutafuta kazi kwa sababu cheti ulichonacho kinawapa shaka waajiri, hivyo hili ni jambo muhimu mno la kuzingatia katika kuhakikisha kuwa unapata chuo kinachouzika kwa haraka zaidi.

Ikiwa na maana kwamba iwapo utasoma kwenye moja ya vyuo hivi basi ni rahisi zaidi kuonekana na kupokelewa na waajiri pindi unapoingia kwenye soko la ajira kwani unakuwa umesoma kwenye vyuo vinavyotambulika duniani. Jumla ya kanda nane zimejumuishwa kwenye utafiti huu uliofanywa na shirika la utafiti wa vyuo vikuu bora duniani la Global Rankings.

 Africa

Tukianza na nyumbani Afrika utafiti huu umebainisha kuwa kwasasa vyuo vikuu vitano ambavyo mwanafunzi yeyote kutoka eneo lolote duniani anaweza kwenda kusoma na akafanikiwa kupata kazi kirahisi ni pamoja na hivi vifuatavyo:

Chuo kikuu cha, Cape Town, kikifutiwa na vile vya Witwatersrand, Stellenbosch, Kwazulu-Natal huku nafasi ya tano ikishikwa na Chuo Kikuuu cha Pretoria vyote kutoka nchini Afrika Kusini. Hii inaonyesha kuwa ni kwa namna gani taifa hili limeweza kujizatiti kwa vyuo vyake vyote kuwa kwenye tano bora ya barani Afrika.

Hata hivyo, hii imekuwa ikitegemeana na utafiti wenyewe kwani tumeshuhudia utafiti mwingine ukivisukumia mbali vyuo hivi vya Afrika Kusini na kuvichukua vile vya Misri na Ghana bila kusahau Makerere kutoka nchini Uganda.

Asia

Kwa upande wa bara hili, vyuo vilivyoingia na kuonekana kuwa bora zaidi ni pamoja na vyuo vikuu vya Tokyo na Kyoto vyote vya nchini Japan. Vingine ni Chuo cha Kimataifa cha Singapore cha nchini Singapore, Chuo Kikuu cha Hong Kong kilichopo Hong Kong na nafasi ya tano ikishikwa na Chuo Kikuu cha Seoul National cha Korea Kusini.

Visiwa Vya Caribbean

Huku kuna vyuo vikuu vya Puerto Rico at Mayaguez, Universidad de Puerto Rico, Puerto Rico Rio Piedras vyote vya nchini vnapatikana nchini Poerto Rico vingine katika nafasi ya nne na ya tano ni Chuo Kikuu cha The West Indies cha Jamaica na Chuo Kikuu cha La Habana – Cuba.

Amerika ya Kati

Hapa kuna vyuo vikuu vya Costa Rico, Nacional vyote vya nchini Costa Rico vingine ni  Rafael Landíva kilichopo Guatemala, El Salvador, Centroamericana José Simeón Cañas vyote vinapatikana nchini El Salvador.

Ulaya

Bara hili limekuwa pia likiongoza kwa kutajwa kuwa na vyuo vikuu bora duniani, hata hivyo kwenye orodha hii vilivyopenya ni vitano pekee ambavyo ni Cambridge, Oxford, Imperial College London vyote vya nchini Uingereza; huku nafasi ya nne ikishikwa na Chuo Kikuu cha ETH Zurich – Swiss Federal Institute of Technology cha Swizerland huku UCL (University College London) cha Uingereza kikishika nafasi ya tano.

Amerika ya Kusini

Vyuo vikuu vya Federal de Sao Paulo, Federal do Rio de Janeiro vya Brazil, Buenos Aires cha Argentina, Estadual de Campinas cha Brazil na Pontificia Universidad Catoilca kilichopo nchini Chile.

Amerika ya Kaskazini

Kama kawaida hapa lazima utakikuta chuo kikuu cha Harvard, Massachusetts Institute of Technology (MIT), Stanford, California Institute of Technology (Caltech) California, Berkeley (UCB) vyote hivi vinapatikana nchini Marekani.

Australia

Kuna vyuo vikuu vya Melbourne, Sydney, The Australian National University,   The University of Queensland na Chuo Kikuu cha  New South Wales vyote vya nchini Australia.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles