24.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

Juisi ya limao husaidia kuondoa mchanga katika figo

Limao
Limao

Na Herieth Faustine,

LIMAO ni tunda dogo ambalo hupendelewa kutumiwa katika mapishi mbalimbali kwa ajili ya kunogesha na kukata shombo katika vyakula kama vile samaki au nyama.

Asili ya tunda hili limetoka katika bara la Asia ambapo katika karne ya 16 lilitumika kama dawa baada ya mabaharia waliokuwa wakivuka bahari ya Pasifiki na Atlantiki kuugua ugonjwa wa kiseyeye.

Licha ya kuwa tunda kama matunda mengine limekuwa haliliwi sana kutokana na kuwa na ladha ya uchachu.

Licha ya uchachu pia lina asili ya asid ya sitriki ambayo huzalisha vitamin C ambayo husaidia kuzuia baridi na homa.

Tunda hili pia lina kitu muhimu ambacho husaidia kuondoa sumu mwilini na kupigana na kansa mbalimbali.

Huzuia matatizo ya kisukari, kufunga choo, shinikizo la juu la damu na husaidia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula kufanya kazi vizuri.

Pia limao husaidia kutibu kikohozi, mafindofindo, mafua, kisukari na pia huleta harufu nzuri kinywani.

Juisi ya limao ina faida nyingi katika mwili wa binadamu kama kuondoa mchanga katika figo.

Kulingana na utafiti uliofanywa na Chama cha Madaktari wa Magonjwa ya Mfumo wa Mkojo cha Marekani (American Urological Association), juisi ya limao au lemonade inaweza kuondoa na kuzuia kujitokeza kwa mawe kwenye figo.

Vilevile juisi hiyo ni dawa nzuri kwa nywele ikipakwa kwenye ngozi kwani hutibu matatizo kama ya mba na kukatika kwa nywele.

Pia juice ya limao hutibu magonjwa mbalimbali ya ngozi kama kuondoa mikunjo na madoa kwenye ngozi.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles