26.9 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

JPM: Sina mpango wa kutoa pesa kwa ajili ya katiba mpya

Bethsheba Wambura, Dar es Salaam

Rais Dk John Magufuli amewataka watu wanaotegemea atoe fedha kwa ajili ya kukaa vikao kujadili masuala ya kubadilisha katiba ya nchi waache kwa sababu hana mpango wala hategemei kufanya hivyo.

Amesema kwa wale wenye fedha wanaotaka kusaidia mpango huo wampatie ili akamalizie mradi wa kujenga reli mpya ya kisasa ya Stiegler’s Gorge.

Ameyasema hayo leo Alhamis Novemba Mosi  alipokuwa akizungumza na washiriki wa kongamano la kuijadili hali ya siasa na uchumi wa nchi lililojumuisha maprofesa na viongozi kutoka katika sekta mbalimbali za serikali na Jeshi, lililofanyika ukumbi wa Nkrumah katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Rais Magufuli amesema amekuwa akipata ushauri kutoka kwa watu mbalimbali kuhusu kubadilisha Katiba mpya wasidhani hajui umuhimu wake ila kwa sasa hana fedha za kufanya hivyo.

“Sitegemei kutoa fedha kwa ajili ya watu kwenda kujadili masuala ya kubadili katiba kama watu wana hizo ela watupe tukamalizie mradi wa Stieglers George,” amesema.

Rais Magufuli amesema hali ya uchumi ya nchi kwa sasa inakuwa kwa asilimia saba na Tanzania ni miongoni mwa nchi Tano za afrika ambazo uchumi wake unakuwa kwa kasi na atasimamia hili ili ikue zaidi ya hapa.

“Nchi yetu ilifika katika hatua  kubwa sana ya rushwa na ndiyo maana  niliamua kujipa kazi kubwa ya kutumbua majipu kwa sababu nilitaka kufikisha nchi sehemu nzuri pamoja na changamoto zake niliapa lazima tutafika tu.

“Katika mambo makubwa ya msingi ni lazima tuyasimamie kwa pamoja kama watanzania bila kujali itikadi zetu za kisiasa na vyama na tusikubali kutumiwa,”amesisistiza Magufuli.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles