26.9 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 21, 2024

Contact us: [email protected]

JPM kuzindua hifadhi ya Burigi Chato

Mwandishi Wetu, Mwanza

Rais Dk. John Magufuli, anatarajiwa kuzindua rasmi hifadhi mpya ya Taifa ya Burigi iliyoko Chato mkoani Geita, wiki ijayo.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamis Kigwangalla amesema hayo jijini Mwanza leo, katika mkutano wa mwaka wa Wahariri na Waandishi waandamizi ulioandaliwa na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (Tanapa).

Amesema ili sekta ya hifadhi iweze kuleta mabadiliko ni lazima jamii wakiwamo wanahabari washiriki katika kutangaza vivutio vya utalii kama njia ya kuongeza idadi ya wageni wa ndani na nje.

“Bila wanahabari sekta ya utalii haiwezi kujulikana hivyo tushirikiane pamoja katika hili.

“Na pia kama mnakumbuka hivi karibuni tumetangaza hifadhi mpya za taifa na Jumanne Rais Magufuli, atazindua hifadhi ya Burigi Chato, lengo ni kuhakikisha wageni waweze kuona maliasili zetu popote pale Tanzania,” amesema Dk. Kigwangalla.

Awali, Kamishna wa Uhifadhi wa Tanapa, Dk. Allan Kijazi, amesema kufanyika kwa mkutano huo wa kila mwaka umeleta mafanikio makubwa ikiwamo kuongezeka kwa idadi ya watalii katika hifadhi za taifa.

Kamishna Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), Dk. Alan Kijazi, akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa  Wahariri na Wanahabari Waandamizi jijini Mwanza. PICHA NA LOVENESS BERNARD

“Wanahabari ni wadau muhimu sana, kwani hata mabadiliko ya mfumo wetu wa uundwaji wa Jeshi Usu ni hatua ya muhimu ambayo itakwenda kuchochea kuongeza chachu ya utalii na kupambana na majangili ambao wamekuwa wakiharibu rasilimali zetu,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles