32.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

JPM KUONGOZA KIKAO SEKTA YA VIWANDA LEO

Na Mwandishi Wetu, Dar


RAIS Dk. John Magufuli, leo anatarajia kuongoza mkutano wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) Ikulu, Dar es Salaam.

Hii itakuwa ni mara ya kwanza, Rais Dk. Magufuli kuongoza kikao hicho tangu alipoingia madarakani mwaka juzi.

Akizungumza na waandishi wa  habari, Dar es Salaam jana, Katibu Mtendaji wa TNBC, Mhandisi Raymond Mbilinyi alisema mkutano huo utajadili mambo mbalimbali.

“Mkutano huu utakaofanyika Ikulu,umeandaliwa baada ya uteuzi wa wajumbe 40; 20, wanatoka sekta binafsi na 20 kutoka sekta ya umma alioufanya rais mwaka jana. “Kikubwa kitakachoangaliwa katika mkutano huu, ni namna gani sekta binafsi inaweza kuunga mkono juhudi za kuifikisha Serikali kwenye maendeleo ya viwada.

“Ajenda kuu itakua ni maendeleo ya viwanda,kutakua na majadiliano kuhusu namna ya kufanya mageuzi ya kilimo, kwa sababu viwanda vingi tunavyoongelea ni vile vya kuongeza thamani mazao,”alisema.

Alisema baraza linathamini nafasi ya wawekezaji nchini, hivyo kila kitu kinapewa kipaumbele

“Baraza litaangalia namna ya kuboresha mazingira ya biashara kwa wawekezaji wa ndani na nje. Lazima ujue taifa unavutiaje watu wenye nia ya kuwekeza kwenye viwanda… iwapo mazingira ni rahisi kiasi gani kwa mtu mwenye  kuanza kuwekeza, sheria, sera zilizopo, taratibu za uanzishaji viwanda, taratibu za upatikanaji ardhi na mambo mbalimbali yanayohusiana na uwekezaji mkubwa na mdogo yote haya, lazima  ujue yakoje,”alisema.

 Kwa kawaida baraza, linakua na wajumbe 40 ambao ni wawakilishi wa sekta binafsi na sekta ya umma ambao kwa pamoja wanajadili maslahi ya pande zote mbili na majadiliano hayo yanaongozwa na rais, ambaye ni  mwenyekiti.

Wajumbe 20 wanaotoka katika sekta binafsi wanaangalia kongani mbali mbali kama viwada vikubwa na vidogo, kilimo, utalii, kampuni kubwa zinazowekeza nchini, wasafirishaji, taasisi za kifedha, taasisi za vyombo vya habari.

Wajumbe 20 wanaotoka katika sekta ya umma wanatoka katika wizara zote zinahusiana moja kwa moja na ukuaji sekta binafsi, mawaziri, Gavana wa Benki Kuu (BoT) na  Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles