23.3 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

JPM avishangaa Vyombo vya Ulinzi nchini kushindwa kukamata dhahabu iliyokamatwa Kenya

Betshsheba Wambura, Dar es Salaam

Rais Dk John Magufuli amevishangaa vyombo vya ulinzi na usalama kwa kushindwa kukamata na dhahabu na fedha zilizoibiwa hapa nchini hadi zikakamatwa na vyombo vya ulinzi na usalama vya Kenya.

Magufuli amevihoji vyombo hivyo leo Jumatano Julai 24, wakati wa makabidhiano ya dhahabu iliyokamatwa nchini Kenya na kuwasilishwa  na Mjumbe Maalum wa Rais Kenyatta yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.

“Wakupongezwa kwa hili ni vyombo vya ulinzi na usalama vya Kenya, najua wakuu wa vyombo Tanzania mpo hapa, lazima niwatandike hapa mbele za watu, kwasababu vitu vimetoka Mwanza vimekamatiwa Kenya, je zilipobebwa Mwanza na Kilimanjaro vyombo vyetu vilikuwa vinafanya nyinyi?

“Je vilishirikiana na huyu muhalifu au vilimuachia, je dhahabu ngapi zimesafirishwa bila watuhumiwa kushikwa? Hili nawaachia nyinyi, mnafanya kazi nzuri ila inawezekana kuna mahali hamfanyi kazi vizuri nah ii inadhihirisha aibu kwa vyombo vyetu na niwaombe mshirikiane, kila mtu asifanye kivyake.

 “Na mimi nitaandika barua rasmi ya kuvipongeza vyombo vya ulinzi na usalama vya Kenya kwa niaba ya Watanzania kwasababu wamefanya kazi nzuri kama wasingezikamata hizi mali leo tusingekuwa hapa, askari walioshiriki katika hili nitafanya mango nione namna ya kuwazawadia wakiwa hukohuko Kenya,” amesema Rais Magufuli.

Dhahabu kilo 35.34 zilizoibiwa hapa nchini na kukakamatwa nchini Kenya.
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles