Shule, vituo vya afya visivyo na vyoo bora marufuku kutoa huduma Tanga

0
743

Amina Omari-Tanga

Serikali mkoani Tanga imepiga marufuku vituo vya Afya, ofisi za umma na shule ambazo hazina huduma ya vyoo Bora kuendelea kutoa huduma.

Agizo hilo limetolewa na Kaimu Katibu Tawala Arbogast Kimasi wakati akifungua kikao kazi cha kubadilishana uzoefu katika utekelezaji wa kampeni ya usafi wa mazingira mkoani humo.

Amesema kuwa maeneo hayo ndio yanayoongoza kwa kuwa na huduma duni za usafi wa vyoo licha ya kukutanisha watu wengi.

“Tunapigana na kudhibiti milipuko ya magonjwa hivyo ni marufuku kwa maeneo hayo kufunguliwa na kuanza kutoa huduma Kama hayana vyoo Bora na vinavyozingatia usafi” amesema.

Kwa upande wake Afisa afya Mkoa Dk Jumanne Magoma amesema kuwa kikao hicho kimelenga kuja na mpango mkakati wa kudhibiti magonjwa ya milipuko pamoja na matumizi ya vyoo Bora katika kaya.

Amesema kuwa licha ya takwimu za vyoo Bora kuongezeka kutoka asilimia 54% hadi kufikia asilimia 59% bado Kuna jukumu la kuhakikisha uhamasishaji kwa jamii unaendelea

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here