Waandishi wetu – Iringa |
RAIS Dk. John Magufuli, amesema atahakikisha kabla ya kipindi chake cha urais hakijaisha, anapandisha mishahara ya watumishi wa umma.
Amesema atapandisha mishahara kwa kiwango kinachoridhisha na si cha Sh 10,000.
Akizungumza jana wakati wa maadhimisho ya sherehe za Mei Mosi mkoani hapa, Rais Magufuli, alisema nyongeza ya mwaka ya mishahara itaendelea kama kawaida.
“Kwa bahati mbaya, leo Dk. Msigwa (Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi – TUCTA, Dk. Yahya Msigwa), amenichomekea kuwa Moshi niliahidi, lakini sikuahidi kwa sababu naikumbuka hotuba yangu, leo ndiyo ninaweza nikaahidi.
“Kama miradi hii itaenda vizuri na kama wafanyakazi hawa 52,000 tutawaajiri na kuwalipa misharaha vizuri na kama vyama vya wafanyakazi vitaendelea kutoa ushirikiano kwa Serikali ya awamu ya tano na hili nalizungumza vizuri na mninukuu vizuri.
“Kipindi changu cha urais hakitaisha kabla …
Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA.