25.8 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

JPM ATETA NA WASTAAFU VYOMBO VYA USALAMA

 

Na Mwandishi Wetu-DAR ES SALAAM

RAIS Dk. John Magufuli, amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wastaafu wa vyombo vya ulinzi na usalama hapa nchini.

Viongozi hao ni Wakuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Wakuu wa Jeshi la Polisi, Wakuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Wakuu wa Idara ya Uhamiaji, Wakuu wa Jeshi la Magereza na Wakuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.

Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam jana, viongozi hao wastaafu wamemshukuru Rais Dk. Magufuli kwa kuwaita na kufanya nao mazungumzo, ambayo yamewawezesha kubadilishana mawazo na kuimarisha zaidi ushirikiano kati yao na viongozi wa sasa wa vyombo hivyo.

“Tunamshukuru sana mheshimiwa Rais Magufuli na tunampongeza kwa kazi nzuri aliyoifanya, sio jambo la kuficha amefanya kazi nzuri, na kila mmoja wetu amezungumza hilo na tunamtakia kila la heri ili aweze kuendeleza pale alipofika, kwa kweli tumefurahi sana,” alisema Corneli Apson ambaye ni Mkurugenzi Mstafau wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu,  Gerson Msigwa, alisema Rais Dk. Magufuli amekutana na viongozi hao kwa lengo la kubadilishana uzoefu na kujenga ushirikiano imara zaidi kwa viongozi wastaafu na viongozi wa sasa katika kutekeleza majukumu ya ulinzi na usalama wa nchi.

“Rais Magufuli amefurahishwa sana na mwitikio wa viongozi hawa wastaafu wa vyombo vya ulinzi na usalama na amewahakikishia kuwa Serikali anayoiongoza itaendeleza ushirikiano nao ili kunufaika na uzoefu wao,” alisema Msigwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles