23.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

JPM AOMBWA KUSAIDIA MIUNDOMBINU SAGCOT

Na Mwandishi Wetu-DAR ES SALAAM


NAIBU Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Kuendeleza Kilimo Ukanda wa Nyanda ya Juu Kusini mwa Tanzania (SAGCOT), Jennifer Baarn, amemwomba Rais Dk. John Magufuli kuangalia kwa jicho la huruma ushoroba wa kituo hicho ili kufikia Tanzania ya viwanda.

“Namuomba Rais Magufuli kusaidia shughuli za SAGCOT katika ushoroba wa Nyanda za Juu Kusini mwa Tanzania na hasa katika masuala ya miundombinu na shughuli za kongani. Vilevile asaidie watendaji wa Serikali ambao tunashirikiana nao katika kuinua kilimo nchini,” alisema Bi. Jennifer.

Jennifer ambaye anamaliza muda wake katika nafasi hiyo, jana alifanya mazungumzo na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam na kusema kwamba, kitu pekee atakachokikumbuka kwa miaka sita aliyokaa Tanzania ni kufanya kazi na watu wanaopenda kujifunza na kuifikisha Tanzania juu kiuchumi.

“Nitakumbuka vitu viwili, kwanza kufanya kazi. Tena kufanya kazi na watu wanaosoma kwa bidii ili kusaidia maendeleo ya nchi yao katika nyanda mbalimbali. Kingine nitakachokikumbuka ni Bagamoyo, naupenda mji ule mkongwe ambao ilikuwa kama nyumbani,” alisema Baarn.

Aidha, mbali na mafanikio aliyoyapata kwa miaka sita aliyokuwemo kwenye kituo hicho kinachofanya kazi kwa ubia  kati ya sekta binafsi na sekta ya umma, Baarn alisema zipo changamoto kadhaa za kiutendaji ambazo zikipatiwa ufumbuzi, Tanzania itakuwa sehemu salama kwa chakula.

Kwa upande wake Ofisa Mtendaji Mkuu wa SAGCOT, Geoffrey Kirenga, kwa namna alivyofanya naye kazi vizuri, Jennifer alisema hajawahi kumuona mtu anayejituma na kufanya kazi za kusaidia kilimo kukua kama yeye.

SAGCOT inasimamia kilimo katika ukanda wa nyanda za juu kusini ambapo inagusia mikoa kadhaa kuanzia Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Iringa, Njombe, Mbeya, Songwe, Lindi na Mtwara pamoja na Ruvuma.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles